Kuanza kwa kongamano la kimataifa na kitamaduni Ruhu Nubuwa…

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo (Ewe Zaharaa.. wito wa kujitolea na pambo la mbinguni) kwa mwaka wa tatu mfululizo, Alasiri ya siku ya Alkhamisi ya tarehe (22 Jamadal Thani 1440h) sawa na (28 Februari 2019m) limeanza kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwa, linalo simamiwa na idara ya shule za wasichana Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kama sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s), ndani ya ukumbi mkuu katika kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s) ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhudhuriwa na watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

Hafla ya ufunguzi wa kongamano imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) na katibu wake mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) pamoja na idadi kubwa ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, baada ya kusomwa Quráni ya ufunguzi na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashaidi wa Iraq na kusikiliza wimbo wa Atabatu Abbasiyya, kulikua na ujumbe kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), alianza kwa kutoa pongezi kwa waislamu wote na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kwa kuadhimisha kuzaliwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s), akamuomba Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa baba yake na mume wake na watoto wake na umri wake alioishi pamoja na mbora wa Manabii na Mbora wa Mawasii atushushie neema na Baraka za kudumu na atutunuku shifaa yake siku ambayo tutaihitajia zaidi.

Kisha likafuata tukio la Quráni lililofanywa na maahadi ya Quráni kitengo cha wanawake, halafu likafuata igizo la wanafunzi wa shule ya Nuru Abbasi (a.s), lililo onyesha subira ya mototo wa shahidi, na namna alivyo fanya bidii katika masomo na kupambana na hali yake ya uyatiba na kuifanya kuwa ni fahari kwake.

Halafu mshairi Dokta Ahmadi Alyawi akaimba kaswida murua iliyo burudisha masikio ya wahudhuriaji kuhusu fadhila na utukufu wa Fatuma Zaharaa (a.s).

Mashahidi nao walipewa nafasi katika kongamano hili kwa kuwapa zawadi wajane na wakina mama wa mashahidi walio jitolea nafsi zao kwa ajili ya taifa hili tukufu.

Baada ya hapo wahudhuriaji wakaelekea katika ufunguzi wa maonyesho ya kazi bora za sanaa zilizo shinda katika shindano lililoendeshwa na kamati ya maandalizi ya kongamano, shindano la kazi za sanaa: (Kazi bora ya kiufundi, hati bora, ubao mzuri wa kiufundi, na picha bora).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: