Atabatu Abbasiyya tukufu imesisitiza kua milango yake iko wazi kwa watafiti wa sekta ya faharasi na usanifu…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imesisitiza kua milango yake iko wazi kwa watafiti wa sekta ya faharasi na usanifu, maadam wanafanya kazi ya kuhakiki vifaa na kuratibu maarifa sambamba na kumiliki faharasi ya kisasa zaidi, hayo yamesemwa na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi na rais wa kitengo cha habari na utamaduni Sayyid Liith Najmu Mussawi katika ujumbe aliotoa kwenye hafla ya kufunga kongamano la kimataifa la kwanza kuhusu taaluma za maktaba, lililo fanywa chini ya anuani isemayo: (Kuratibu maarifa katika sekta ya namba) Alasiri ya Alkhamisi (22 Jamadal Thani 1440h) sawa na (28 Februari 2019m), miongoni mwa aliyosema ni: “Miongoni mwa furaha kubwa kwetu ni kukutana pamoja kwa ajili ya kuweka maazimio ya mwisho kwa ajili ya kazi zetu, tumefanya kazi ya kutafuta njia bora ya kuratibu uwelewa wa maktaba, unao endana na maendeleo ya kisasa yaliyo gunduliwa na watafiti wa taaluma za maktaba, pamoja na ugumu wa mazingira ya maktaba za sasa, taarifa zinapatikana kwa shida pamoja na kuwepo njia tofaoti za kupata taarifa kama vile video, audio na picha”.

Akaongeza kua: “Lengo letu ni kuleta maendeleo katika sekta ya faharasi na usanifu, tuzikumbushe nafsi zetu kua maendeleo tunayo yaona hayakuja siku moja, yamepatikana baada ya juhudi kubwa za miaka mingi, tunatakiwa kukusanya nguvu na kufanya kazi kwa bidii sambamba na kuwasaitia wataalamu wa mambo ya maktaba na watafiti”.

Akaendelea kusema kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha faharasi na usanifu inafanya kazi kubwa katika sekta ya faharasi, na inatilia umuhimu kushiriki wataalamu wake katika makongamano na mikutano mbalimbali ya wabobezi na taasisi za wadau wa mambo ya maktaba, na kongamano hili ni kielelezo cha ushirikiano na kutoa fursa kwa wadau, na kuweza kubadilishana elimu kwa urahisi na kuokoa muda ambao wangeweza kuutumia kwa jambo hili”.

Akasisitiza kua: “Hakika makongamano haya yanaumuhimu mkubwa sana, na sisi tunawaahidi kua milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu iko wazi kwa ajili ya mambo haya na mengineyo, maadam yanakusudia kuhakiki vifaa na kuratibu maarifa na hatimae kumiliki faharasi ya kisasa zaidi”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunaushukuru uongozi wa chuo kikuu cha Mustanswiriyya, na wakuu wa vitengo vyake na marais wa maktaba katika kitivo cha adabu, wamekua msaada mkubwa sana kwetu katika kufanikisha kongamano hili, pia shukrani za dhati ziende kwa muungano wa waarabu kwa ajili ya maktaba na taaluma kwa ushiriki wao mkubwa kwenye kongamano hili tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: