Maoni katika picha
Familia za mashahidi zimepewa zawadi katika hafla ya ufunguzi wa kongamano la Ruhu Nubuwa awamu ya tatu, kulikuwa na zawadi za madiyya na maanawiyya, kazi ya kutoa zawadi imefanywa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahamadi Swafi (d.i) na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) pamoja na mjumbe wa kamati ya uongozi bwana Jawadi Hasanawi.
Utowaji wa zawadi kwa familia za mashahidi wa hashdi Sha’abi ni sehemu ya kuwaenzi mashahidi hao kwa kujitolea kwao kulinda taifa na maeneo matakatifu, zawadi hizo hukabidhiwa wazazi, wake na watoto walio jitolea wapenzi wao kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Iraq, na kuibakisha ardhi ya Iraq na maeneo matakatifu yakiwa twahara bila uchafu wa magaidi.
Mjumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na msimamizi wa kongamano hili bwana Jawadi Hasanawi amesema kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inajitahidi kutumia kila fursa kuonyeha namna inavyojali damu takatifu iliyo mwagika kwa ajili ya kulinda taifa na maeneo matukufu, miongoni mwa fursa hizo ni kongamano la Ruhu Nubuwa, tumetenga muda wa kutoa zawadi kwa familia za mashahidi kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano, hakika zawadi tunazo wapa ni ndogo sana ukilinganisha na kujitolea kwao”. Akasisitiza kua: “Hakika familia za mashahidi ni dhima kwetu, kuwapa zawadi kama hivi kunawafanya mayatima wao wahisi kuwa kuna watu wanao waangalia, jambo hilo linasaidia kuwajenga kifikra katika maisha yao”.
Kwa upande wa familia za mashahidi zimetoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na kamati ya maandalizi ya kongamano la Ruhu Nubuwa kwa kuwapa zawadi, wakasema kua hili sio jambo geni kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kutoa zawadi kwa familia za mashahidi na majeruhi, hakika imekuwa ikiwakumbuka kila wakati.