Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) leo (23 Jamadal Thani 1440h) sawa na (1 Machi 2019m) chini ya uimamu wa Shekh Abdulmahdi Karbalai ameongelea vipengele vingi vya kimaadili na kimalezi vinavyo gusa mazingira halisi ya maisha, miongoni mwa vipengele alivyo sema ni:
- - Tunaiomba serikali ya Iraq na taasisi za kimataifa kuwasaka magaidi wa Daesh na kuwahukumu kwa jinai zao.
- - Tunaungana na ndugu zetu raia wa Iraq wa kabila la Aizidiy.
- - Tunaitaka serikati ya Iraq kuchukua hatua za makusudi na kuhakikisha jinai hizi hazijirudii tena kwa raia wa Iraq.
- - Tunaitaka serikali ya Iraq iwashambulie vikali magaidi wa Daesh popote walipo na kuhakikisha hawafanyi jinai zao mahala popote katika taifa hili.
- - Biashara haram ya dawa za kulevya inatishia jamii yetu hasa tabaka la vijana.
- - Madhara ya kutumia dawa za kulevya hayaishii katika kuharibu akili peke yake, bali huharibu afya na utamaduni hasa katika tabaka la vijana.
- - Jambo linalo haribu vijana huwa hatari sana kwa jamii, bali ndio jambo lenye hatari zaidi katika jamii.
- - Tatizo la dawa za kulevya lina sehemu kuu mbili, kwanza upande wa biashara kwa watu wenye nafsi dhaifu, na upande wa pili ni wahanga wanaotumia dawa hizo.
- - Miongoni mwa sababu za janga hili ni kutovipa uwezo kamili vyombo vinavyo pambana na dawa za kulevya.
- - Miongoni mwa sababu za janga hili ni udhaifu wa vyombo vinavyo pambana na dawa za kulevya.
- - Kuingiliwa utendaji wao na watu wenye mamlaka juu yao ni kudhoofisha mfumo wa sharia.
- - Sababu ya kuenea tatizo hili ni ukosefu wa ajira na ufakiri pamoja na kuwepo watu wanaotaka mali za haraka kwa kufanya biashara haram ya dawa za kulevya.
- - Kukosekana kwa ajira na kukata tamaa ya maisha ni miongoni mwa sababu za watu kujiingiza katika biashara ya dawa za kulevya.
- - Marafiki waovu na matatizo ya kifamilia na kijamii pamoja na uwelewa mbaya wa uhuru pia ni miongoni mwa sababu za kuenea biashara ya dawa za kulevya.
- - Inatakiwa kuunganisha nguvu ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii katika kueleza madhara ya janga hili.
- - Miongoni mwa sababu za kuenea dawa za kulevya ni udhaifu wa taasisi za serikali.
- - Taasisi za serikali zimejikita katika maswala ya vita na siasa pamoja na kulinda maslahi binafsi zaidi kuliko maslahi ya umma.
- - Kila mtu anawajibu wa kupambana na janga hili mbele ya Mwenyezi Mungu.
- - Kiongozi wa familia anawajibu wa kulinda watu wa familia yake wasiwe waovu na wasiwe na marafiki wabaya.
- - Shule na vyuo vikuu vinawajibu wa kufundisha madhara ya biashara ya dawa za kulevya.
- - Umuhimu unaowekwa katika maswala ya elimu za kisekula unatakiwa pia uwekwe katika kutoa malezi mema kwa vijana wetu.
- - Tunatoa wito kwa taasisi za serikali kutengeneza nafasi za kazi kwa wingi sambamba na ongezeko la ukosefu wa ajira.
- - Tunatoa wito wa kuwatambua wasio kua na kazi na kuweka utaratibu mzuri wa kutumia mali kwa usahihi.
- - Tunatoa wito wa kushirikiana na vyombo vinavyo pambana na dawa za kulevya na kuacha kuvizuwia kufanya kazi yake.
- - Tunatoa wito wa kuundwa sharia maalumu za kupambana na dawa za kulevya.