Katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s): Arshu Tilawa inaendeleza mahafali za Qur’ani...

Maoni katika picha
Mahafali za usomaji wa Qur’ani zinazo ratibiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani katika Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya zinaendelea kufanyika kila jioni ya siku ya Ijumaa chini ya mradi wa Arshi Tilawa, katika mahafali hizo hualikwa taasisi za Qur’ani kutoka ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala.

Kamati imealika taasisi za Qur’ani kutoka mkoa wa Waasit wilaya ya Kuut kuwa wageni katika mahafali ya Arshu Tilawa ya wiki hii, ambazo hufanywa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kushiriki jopo la wasomaji wa Qur’ani, waliosoma Qur’ani katika mahafali hii ni: msomaji wa Atabatu Abbasiyya Shekh Ali Saaidiy, Buraqu Muniri Abadi, mmoja wa wahitimu wa kozi ya pili, msomaji wa kitengo cha Qur’ani tukufu katika kamati ya Hashdi Sha’abi, Mustwafa Ma’yuuf kutoka mkoa wa Waasit, Mustwafa Kaatw’i Albudiri, mmoja wa wasomaji wa mradi wa wasomaji wa taifa kutoka katika umoja wa wasomaji wa Qur’ani tukufu wilaya ya Aalu Budair katika mkoa wa Diwaniyya.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani ya Atabatu Abbasiyya tukufu imesha fanya miradi mingi ya Qur’ani tukufu, na miongoni mwa miradi hiyo ni huu wa Arshu Tilawa, nao unalenga kunufaika na vipaji vya usomaji wa Qur’ani vya wairaq, na kuvionyesha katika ulimwengu wa kiislamu, sambamba na kulea vipaji hivyo chini ya utaratibu maalumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: