Chuo kikuu cha Ameed ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimekuwa mwenyeji wa kikao cha usomaji wa Qur’ani tukufu ambacho kipo katika ratiba ya kongamano ya Ruhu Nubuwa, katika kikao hicho wameshiriki wasomaji wa Qur’ani tukufu kutoka katika mji wa Karbala na wengine kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Iran na Afghanistan, imeratibiwa na idara ya shule za Alkafeel katika kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s) kwa kushirikiana na shule za wasichana za Al-Ameed.
Katika hicho kimepata mahudhurio makubwa ya wageni wa kongamano, wasomaji wameburudisha masikio ya wahudhuriaji kwa visomo murua vya kitabu cha Mwenyezi Mungu, hali kadhalika kulikuwa na tenzi za kumsifu bibi Fatuma Zaharaa (a.s).
Washiriki wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kufanya kikao kama hiki cha usomaji wa Qur’ani, kwani vikao vya aina hii vinawatambulisha wakazi wa Karbala, pia ni fursa ya kutambulisha harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye upande wa usomaji wa Qur’ani katika kitengo cha wanawake.
Kumbuka kua idara ya shule za Alkafeel za Qur’ani katika kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s), inafanya juhudi za kuendesha vikao vya usomaji wa Qur’ani tukufu katika kongamano la Ruhu Nubuwa, na hufanya semina za ngazi ya chini na ngazi ya juu pamoja na vikao vya kufundisha hukumu za usomaji, sauti na naghma, sambamba na miradi mikubwa ya Qur’ani inayo lenga kuandaa wasomaji wa kike wenye uwezo mkubwa wa kusoma Qur’ani na kuelewa fani zake.