Mradi wa kufuta ujinga katika Atabatu Abbasiyya tukufu umeanza kusajili wanafunzi wa masomo ya msingi…

Maoni katika picha
Miongoni mwa miradi yake ya elimu inayo endelea kwa lengo la kuwasaidia wasiokua na elimu, watu wasiojua kusoma na kuandika, na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana siku za nyuma, mradi wa kufuta ujinga, ambao ni kati ya miradi inayo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, imetanganza kuanza kwa usajili wa masomo ya ngazi ya msingi, kwa lengo la kupunguza idadi ya wasiojua kusoma na kuandika hapa nchini, na imetoa wito kwa kila anaye taka kujiandikisha afanye haraka.

Mradi huu unafanywa katika kipindi ambacho kunaongezeko la watu wasiojua kusoma na kuandika hapa nchini, wakati zama hizi kusoma na kuandika ni jambo la lazima katika maisha, pamoja na kua ndio njia muhimu ya kuwasiliana na watu katika jamii.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa walimu mahiri wenye uzowefu mkubwa wa kufundisha masomo hayo.

Masharti ya kujiunga na masomo ni:

  • 1- Muombaji asiwe chini ya miaka (18).
  • 2- Awe hajui kusoma na kuandika.

Tunapenda kufahamisha kua atakaye hitimu masomo haya atapewa cheti cha kuthibitisha kuwa anajua kusoma na kuandika kinacho tambuliwa na wizara ya malezi na elimu ya Iraq.

Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu kwa namba zifuatazo: (07602323721 / 07723771314).

Kumbuka kua mradi huu ulianza kutekelezwa baada ya kuruhusiwa na wizara malezi ya Iraq, kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala, na unaendeswa na walimu mahiri waliopewa mafunzo maalumu ya ufundishaji wa masoma hayo, sambamba na kuandaliwa sehemu maalumu za kufundishia, zimechaguliwa husseiniyya na majengo kadhaa ndani ya mkoa wa Karbala na kutumiwa kama madarasa, cheti cha kufuta ujinga kinatolewa baada ya kumaliza hatua ya msingi ambayo ni sawa na tarasa la nne katika shule ya msingi, mtihani wa kuhitimu masomo hayo ya msingi unatolewa na wizara ya malezi na wizara hiyo hiyo ndio inayotoa vyeti, na vinatambuliwa na sekta zote za serikali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: