Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhwiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) tumeigawa sehemu nyingi katika mradi wa kuweka marumaru, kwa namna ambayo hatuzuwii mazuwaru kuendelea na ibada zao, kila sehemu ikikamilika tunaifungua na kuhamia sehemu nyingine, tutaendelea kufanya hivyo hadi tumalize kuweka marumaru katika uwanja wote wa haram tukufu”.
Akaongeza kua: “Kazi inaendelea vizuri tunatarajia kumaliza ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu, kazi hii inajumuisha uwekaji marumaru majengo ya chini, kwenye mitambo ya umeme, sehemu za usambazaji wa maji na sehemu ya taa na zinginezo, pamoja na kazi zingine za awali kama vile kutoa marumaru za zamani na kurekebisha sehemu zilizo haribika”.
Kuhusu wasifu wa marumaru amesema kua: “Marumaru ni za kawaida ambazo hupatikana kwa nadra (Malt Oksi), zinamazuri mengi, muhimu ni kwamba ni marumaru za kawaida zenye rangi nzuri na uwezo mkubwa wa kuvumilia mazingira, zinamuonekano mzuri na zinaupana wa (sm 4) takriban.
Kumbuka kua mradi wa kuweka marumaru kaika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ni mradi unaokamilisha miradi iliyotekelezwa siku za nyuma, unafanyika baada ya kuharibiba marumaru za zamani na kuharibu mandhari ya haram kutokana na ukongwe wake, kwani zilikua zina Zaidi ya miaka mia moja tangu ziwekwe kwenye haram tukufu, pia kwa ajili ya kupendezesha sehemu hii tukufu ambayo ni miongoni mwa sehemu za peponi, kwa namna ambayo itawafurahisha mazuwaru watukufu.