Walimu na wanafunzi wa kitivo cha Tarbiyya katika chuo kikuu cha Bagdad wamekua wageni wa baba wa ukarimu Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudumiwa na idara ya mahusiano na vyuo vikuu chini ya ratiba maalumu iliyo kuwa na vipengele vifuatavyo:
- - Kufanya ziara ya pamoja katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Kutembelea vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kikiwemo kitengo cha zawadi na nadhiri, walipewa maelezo kamili kuhusu utaratibu wa kupokea zawadi na uwekaji wa nadhiri katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na baada ya kupokelewa zawadi hupelekwa wapi na hutumika vipi, walitembelea maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya na kuangalia vitu vinavyo husiana nayo, hasa sekta ya utafiti na uwandishi wa kazi za chuo, pamoja na vitabu ambavyo vinawafaa wanafunzi, walimu na watafiti, hali kadhalika wametembelea kituo cha kibiashara cha Afaaf na vitalu vya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Kufanya kikao cha majadiliano kilicho pewa anuani ya: (Mwanafunzi wa chuo na changamoto za sasa) kilicho hutubiwa na Sayyid Muhammad Abdullahi Mussawi kutoka kitengo cha Dini, akaelezea mambo mengi, akafafanua nafasi ya jamii kwa wanafunzi na vijana wa vyuoni kwa kuzingatia kua wao ni moja ya nguzo muhimu katika jamii, na Marjaa Dini mkuu amesisitiza umuhimu wa kuwajali vijana.
Ziara hiyo ilihitimishwa kwa kutembelea mji wa Sayyid Auswiyaa ambao upo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kupiga picha za ukumbusho.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inavijali sana vyuo vikuu, inamiradi mingi kuhusu vyuo, kuna miradi inayo husu wakufunzi na inayo husu wanafunzi wa vyuo, mradi wa Multaqa Thaqafi ni moja ya miradi inayo endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.