Kitengo cha idara ya ubora cha baraza la mawaziri chasema: Tunatarajia kudumisha uhusiano na hospitali ya rufaa Alkafeel…

Maoni katika picha
Kitengo cha idara ya ubora cha baraza la mawaziri la Iraq kupitia Dokta Yusufu Yaquub kimesema kua: “Tunatarajia kudumisha uhusiano na ushirikiano pamoja na hospitali ya Rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kufanya harakati za pamoja, ikiwa ni pamoja na kufanya warsha za kuongeza ubora katika huduma za ayfa.

Ameyasima hayo katika ujumbe aliowasilisha kwenye warsha ya kuwajengea uwezo wajumbe wa vitengo vya ubora vya mikoani, inayo simamiwa na baraza la mawaziri kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Karbala pamoja na hospitali ya rufaa Alkafeel, chini ya kauli mbiu isemayo: (Ubora ni jukumu la wote), miongoni mwa aliyo sema ni: “Kwaniaba ya baraza la mawaziri na kwaniaba ya kitengo cha ubora natoa shukrani za dhati kwa uongozi wa mkoa wa Karbala na kwa Atabatu Abbasiyya tukufu bila kuisahau hospitali ya rufaa Alkafeel kwa kuwa mwenyeji wa warsha hii, tunatarajia kudumisha uhusiano na ushirikiano katika kuendesha harakati hizi, na hazitaishia Karbala peke yake bali zitaendelea katika miji mingine pia”.

Akabainisha kua: “Kufanya semina za aina hii ni miongone vya vipaombele vya kitengo cha ubora cha baraza la mawaziri, lengo ni kubadilishana uzowefu na kujenga uwezo wa uwelewa wa vigezo vya kimataifa, kutokana na umuhimu wa kuboresha huduma zinazo tolewa na taasisi mbalimbali, pia kuna jambo lingine ni vizuri kulisema, ni kutaka kukidhi vigezo vya kimataifa katika utowaji wa huduma za afya, nalo ni jambo muhimu sana ili tuendane na maendeleo ya dunia ya leo, kama tukifuata vigezo vya kimataifa tutaweza kutoa ushindani katika soko la kimataifa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: