Shamba boy wa Alkafeel wazipamba barabara za Karbala kwa miti ya Akasiya

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kikosi chake cha shamba boy cha Alkafeel inaupamba mji wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) mji mtukufu wa Karbala, na kuufanya uwe na muonekano mzuri wa kijani kibichi kwa kiasi ambacho unaingiza furaha katika nyoyo za mazuwaru watukufu, mradi huu unahusisha barabara zote pamoja na njia ndogo (chochoro), wanapanda miti mizuri inayo endana na hali ya hewa na mkoa huu, miongoni mwa miti hiyo ni miti ya Akasiya ambayo imeoteshwa kwa wingi katika vitalu vya Alkafeel.

Kiongozi mkuu wa utekelezaji wa mradi huu bwana Khaliil Hanuun ambaye ni rais wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kutokana na juhudi tukufu za kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ya kupanda miti katika mji wa Karbala kwa zaidi ya miaka kumi sasa, jambo hilo limetusukuma kutafuta aina tofauti za miti, tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumesha panda sehemu kubwa ya barabara za mji huu, na mti wa Akasiya umechukua nafasi kubwa katika miti iliyo pandwa, kutokana na uzuri wa mti huo na kukua kwake kwa haraka”.

Mhandisi wa kilimo bwana Ahmadi Abdalatifu mmoja wa shamba boy anayefanya kazi katika mradi huu amesema kua: “Kikosi cha shamba boy cha Alkafee kilianza kuotesha miti ya Akasiya yenye muonekano mzuri kwenye vitalu vya muswala Rabii na Khariif, kuanzia uandaaji wa kitalu na kukiwekea mbolea ya Botimosi, kisha kuweka mbegu ambazo huchukua siku arubaini hadi kufikia kiwango ambacho unaweza kwenda kuzipanda sehemu kusudiwa”.

Akaongeza kua: “Kuna aina nyingi za mbegu ya Akasiya zilizo pandwa katika mji wa Karbala, Akasiya ni mti wenye mauwa mazuri na umepandwa sana katika miji tofauti duniani, na inakubali vizuri katika ardhi ya Iraq, kwa hiyo imeoteshwa kwa wingi katika vitalu vya Alkafeel na kuwa wauzaji wakuu wa miti hii hapa Iraq, pamoja na kuisambaza ndani na nje ya mkoa wa karbala”.

Tunapenda kuwajulisha kuwa aina hii ya miti ni mpya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendana na mazingira ya hali ya hewa ya Iraq na inakuwa kwa haraka, imepatikana kutokana na juhudi za shamba boy wa Alkafeel.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tikufu imechukua jukumu la kupanda miti, na imeunda kamati maalumu kwa ajili ya kazi hiyo katika kitengo cha utumishi, asilimia kubwa ya miti inaoteshwa na kikosi cha shamba boy cha Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kamati hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: