Kwa mara ya kumi na nane mfululizo: Maahadi ya Qur’ani tukufu inaendesha semina ya Nuru Zaharaa (a.s) kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya

Maoni katika picha
Miongoni mwa miradi ya Qur’ani inayo lenga kuboresha usomaji wa kitabu za Mwenyezi Mungu semina ya Nuru Zaharaa, Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya inaendesha semina hiyo kwa mara ya kumi na nane mfululizo, kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya, na kushiriki zaidi ya watumishi (20), wanafundishwa kwa nadhariyya na vitendo namna ya usomaji wa Qur’ani kwa muda wa mwezi mmoja kila siku wanasoma kwa muda wa saa moja.

Mkufunzi wa semina hii Ustadh Alaa Dini Hamiri ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Semina hii inakusudia kufundisha usomaji sahihi wa kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu, na inawahusu watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kutoka vitengo tofauti, kwa ajili ya kuwafundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kuanzia matamshi ya herusi, sifa za herufi na hukumu zake”.

Akaongeza kua: “Pamoja na kutofautiana viwango vya elimu lakini tunahakikisha kila mtu anafaidika na masomo haya, kupitia sherehe nzuri inayo endana na kiwango cha elimu ya kila mtu”.

Akaendelea kusema: “Semina hii itadumu kwa muda wa siku thelathini, kila siku wanasoma kwa muda wa saa moja, tunapata ushirikiano mzuri sana kutoka kwa watumishi wa Ataba na wana mwitikio mkubwa wa kushiriki katika semina hii”.

Kwa upande wa wana semina, wamepongeza kufanyika kwa semina hii, na wameipongeza sana Maahadi ya Qur’ani tukufu pamoja na watumishi wake wote kwa kuandaa semina hii na kuwapa nafasi ya kufundishwa usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu, na kazi kubwa wanayo fanya ya kuwafundisha.

Semina hii ni miongoni mwa semina zinazo simamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu, kwa ajili ya kuwafanya watumishi wa Ataba waweze kusoma Qur’ani kwa ufasaha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: