Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika nadwa ya kielimu kuhusu athari ya teknolojia katika kuandaa maarifa na anuani za kihistoria

Maoni katika picha
Katika ushiriki wake kwenye nadwa na makongamano ya kielimu, maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya imeshiriki katika nadwa ya kielimu iliyo andaliwa na kitivo cha tarbiyya cha wasichana / kitengo cha historia katika chuo kikuu cha Bagdad.

Nadwa hii ni moja ya nadwa nyingi zinazo fanywa na kitengo hiki, na imefanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Athari ya teknolojia katika kuandaa taarifa za kihistoria) na anuani isemayo: (Elimu ya teknolojia).

Katika ufunguzi wa nadwa, rais wa kitengo cha historia Dokta Khadhar Abduridhwa Alkhafaji, amewakaribisha watafiti na wageni wote kwa ujumla, akasema kua: “Kutumia teknolojia za kisasa katika ufundishaji na usomaji kuna umuhimu mkubwa kwenye vyuo vikuu, pamoja na mazingira inayo pitia Iraq wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu pamoja na sekta zisizokua za serikali, zimetoa kipaombele zaidi katika kuboresha elimu kwa kutumia teknolojia mbalimbali zinazo rahisisha kubadilishana elimu na kuwasiliana kwa urahisi”.

Nadwa hii imeshuhudia uwasilishwaji wa tafiti mbalimbali kutoka kwa watafiti tofauti, wakiwemo watafiti wa maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, Ustadh Swabahu Mahadi amezungumzia (Vyombo vya mawasiliano ya kijamii na nafasi yake katika kubaini ukweli / tukio la kutekwa waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Aljeria Mheshimiwa Muhammad Swidiiq bun Yahya kama mfano).

Pia maktaba ilishiriki katika uwasilishaji wa mada kupitia Ustadh Ammaar Hussein Jawaad / mwenye shahada ya masta ya kompyuta, na Ustadh Muhammad Hassan Yusufu / mwenye shahada ya masta ya historia, mada zao zilihusu (Maktaba ya kielektronik katika maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu na nafasi yake katika kutambulisha elimu za kihistoria), wamejikita katika kuelezea umuhimu wa vitabu vya kielektronik katika kutoa elimu ya historia na nafasi ya maktaba ya kielektronik katika kutunza vitabu vya kielektronik.

Kisha yakafanyika majadiliano na kutolewa maoni mbalimbali kuhusu maktaba ya kielektronik ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wahudhuriaji na washiriki wote wamesifu huduma bora inayo patikana katika maktaba ya Atabatu Abbasiyya.

Nadwa ilikuwa na mada nyingi, mada ya kwanza ilihusu mafhumu ya teknolojia kitaalamu, na mada ya pili ilizungumzia namna ya kutumia teknolojia katika masomo ya kihistoria, huku mada ya tatu na ya nne zikitolewa na wakufunzi wa historia katika vyuo vikuu, ambapo walielezea harakati zao katika vitengo vya historia na namna ya kunufaika na mitandao ya kielektronik, uwanja wa teknolojia unanafasi kubwa katika sekta ya makhtutwaat, na mada ya mwisho ilihusu nafasi ya mitandao ya kielektronik kihistoris.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: