Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Ali Sistani imetangaza kua kesho tarehe (9 Machi 2019m) ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Rajabu (1440h).
Hayo yapo katika taarifa iliyo tolewa na ofisi hiyo kwa mtandao wa kimataifa Alkafeel, ifuatayo ni nakala ya taarifa hiyo:
Kwa jina la mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
Haijathibiti kwa Mheshimiwa Sayyid Sistani kuonekana mwezi wa Rajabu kwa macho baada ya kuzama jua la siku ya Alkhamisi (29/ Jamadal Thani/ 1440h) hapa Iraq na miji jirani, kwa hiyo siku ya Jumamosi itakua siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Rajabu.
Mwezi wa Rajabu ni mwezi wa Mwenyezi Mungu mtukufu, nao ni miongoni mwa miezi mitukufu zaidi, pia ni mwezi wa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), ni mwezi wa Istighfaar, katika siku ya kwanza imesuniwa kufanya ibada nyingi, miongoni mwa ibada hizo ni:
Kwanza: Kufunga, imepokewa kuwa Nabii Nuhu (a.s) alipanda safina yake katika siku hiyo na akawaambia watu wake wafunge, atakaefunga siku hiyo atawekwa mbali na moto kwa masafa ya mwaka mmoja.
Pili: Kuoga.
Tatu: Kumzuru Imamu Hussein (a.s), imepokewa kutoka kwa Bashiri Dahani kutoka kwa Swadiq (a.s) anasema: (Atakae mzuru Hussein bun Ali (a.s) katika siku ya kwanza ya mwezi wa Rajabu Mwenyezi Mungu atamsamehe dhambi zake).