Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa…

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) leo (30 Jamadal Thani 1440h) sawa na (8 Machi 2019m) chini ya uimamu wa Sayyid Ahmadi Swafi amezungumza vipengele vingi vya kimaadili na kimalezi, vinavyo endana na mazingira halisi tunayo ishi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

 • - Yapasa kupiga kengele ya tahadhari kutokana na hatari ya mmomonyoko wa baadhi katika taifa letu.
 • - Kuna misingi ya kimaadili inatakiwa ishamiri katika jamii lakini kwa bahati mbaya imeanza kupotea, na ajabu Zaidi kuzuwia isipotee ni jambo gumu sana.
 • - Aibu ni aina ya hisia na sio mateso.
 • - Haya ni hali ya kuona aibu pindi unapofanya jambo lisilopendeza katika jamii.
 • - Kadri mtu anavyokua na heshima kubwa ndio hisia za haya inavyo ongezeka mbele ya jamii.
 • - Tunaishi katika zama ambazo kuna watu wanataka kuondoa hisia za haya.
 • - Kuna watu wanatumia msamiati wa uhuru kuondoa hisia za haya kwa vijana na wasichana.
 • - Jamii inatakiwa ilinde hisia za aibu wala isiruhusu yeyote kuondoa hisia hizo.
 • - Kuna watu wanataka kuliingiza taifa katika vurugu zisizo kua na mwisho.
 • - Uhuru unamisingi yake, unaheshimu familia, jamii na tamaduni za watu.
 • - Lazima kuwe na kitu kinacho linda jamii isiangamie, kuna mifano mingi ya mmomonyoko wa maadili.
 • - Wananchi wa Iraq wanamisingi ya kimaadili, wanachuoni, familia tukufu na vijana ambao wako tayali kufa kwa ajili ya kutekeleza fatwa, na wakina mama jasiri waliolea majemedari na kuwahimiza kulinda taifa lao.
 • - Olewenu tena olewenu kudanganyika na maneno yasiyokua na maana.
 • - Inaumiza sana nafsi zetu kuona jamii inaanza kua na muelekeo usiofaa.
 • - Wenye mamlaka wanaupungufu katika kulinda jamii isiangamie.
 • - Tatizo kubwa watu wenye mamlaka wako mbali na jamii.
 • - Tunatakiwa kuamka na kujenga kizazi kitakacho jenga taifa hili, uhuru ni jambo zuri lakini chini ya misingi na kanuni zake.
 • - Kunabaadhi ya watu wanataka kuharibu jamii.
 • - Lazima tusimame imara kuzuwia uharibifu wowote unaotaka kuharibu utambulisho na utukufu wetu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: