Mtume (s.a.w.w) anasema: (Tambueni Rajabu ni mwezi wa Mwenyezi Mungu, nao ni mwezi mtukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, watu wa zama za ujinga walikuwa wanautukuza, na ulipokuja uislamu umeendelea kuutukuza).
Hakika mwezi huu ni mwezi mtukufu, na mwezi bora wa kusoma dua, kwa hiyo mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) hupenda kuupokea wakiwa wanasoma dua na kutawasal kwa viumbe bora Zaidi ambao ni Mtume Muhammad (s.a.w.w), Ali, Fatuma, Hassan na Hussein (a.s), wamemuomba Mwenyezi Mungu ailinde Iraq na kila balaa na awarehemu mashahidi na kuwapa subira familia zao, pamoja na kuwaponya haraka majeruhi, na aufanye mwezi wa Rajabu kua mwezi wa kheri na Baraka kwa wananchi wote wa Iraq.
Katika mazingira ya kiimani na kwa ajili ya kuwafanyia wepesi mazuwaru watukufu wanaokuja kufanya ziara katika siku hizi, Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimejipanga kuimarisha ulinzi na kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru watukufu.