Mwezi mosi Rajabu ni siku iliyozaliwa nyota ya tano miongoni mwa nyota za Muhammadiyya Imamu Muhammad bun Ali Al-Baaqir (a.s) Baaqir uluumil awalina wal-aakhirina.

Maoni katika picha
Mwezi mosi Rajabu ni siku iliyozaliwa nyota ya tano miongoni mwa nyota za Muhammadiyya Imamu Muhammad bun Ali Al-Baaqir (a.s) Baaqir ulumil-awalina wal-aakhirina aliyezaliwa mwaka wa (57h), akapokelewa na Ahlulbait kwa shangwe na furaha kwani walikua wanasubiri kuzaliwa kwake kuliko bashiriwa na Mtume (s.a.w.w) kwa muda mrefu, anatokana na kizazi kitakasifu, na watu wake walikua watukufu baada ya kuwa na ukamilifu wa kibinaadamu, kifikra, kiitikadi, kiakili na kimaadili.

Imamu Muhammad Baaqir (a.s) ni Imamu wa kwanza aliyezaliwa na wazazi wote wawili wanaotokana na maimamu watakasifu, baba yake ni Imamu Ali Zaunul-Aabidina mtoto wa Imamu Hussein mtoto wa Imamu Ali mtoto wa Abu Twalib (a.s), na mama yake ni bibi mtakasifu Fatuma mtoto wa Imamu Hassan mtoto wa Imamu Ali mtoto wa Abu Twalib (a.s), anaitwa “Ummu Abdullahi”, alikua ni miongoni mwa wanawake watakatifu wa bani Hashim, Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alikua anamwita Swidiqah, Imamu Abu Abdillahi Swadiq (a.s) anasema kua: (Swidiqah hakua na mfano wake katika kizazi cha Hassan), yatosha fahari kwake kua anatokana na pande la damu ya Mtume (s.a.w.w), na kwamba amekulia katika nyumba alizo amrisha Mwenyezi Mungu zijengwe na litukuzwe jina lanke ndani ya nyumba hizo, miguu yake mitakasifu ndio iliyomlea Imamu Baaqir (a.s).

Jina lake ya kuniya anaitwa (Abu Jafari) na hana kuniya nyingine zaidi ya hiyo. Majina ya laqabu ni: (Al-Amiin, Shabiih –kwa sababu alikua anafanana na babu yake (s.a.w.w)- Shaakiru, Haadi, Swaabir, Shaahid, Baaqir –hii ndio laqabu inayo julikana zaidi-) yeye na mwanae Imamu Swadiq huitwa mabaaqir wawili (Baaqiraini) na huitwa pia maswadiq wawili (Swadiqaini).

Imamu Baaqir (a.s) alisoma elimu na maarifa kutoka kwa baba yake Imamu Zainul-Aabidina (a.s), hadi akafika kiwango cha juu kabisa katika elimu, akawa kama alivyo bashiriwa na babu yake (s.a.w.w) aliye mpa jina la sifa (laqabu) aliposema: (Hakika atapata elimu kwa haraka) alipo bashiri kuzaliwa kwake na kazi kubwa atakayo fanya katika kufundisha elimu ya sheria katika zama ambazo uislamu utaenea katika nchi nyingi, na kutakua na mwingiliano wa tamaduni za watu na kuingiliana mambo ya kimila na kiislamu, alijulikana kwa ufasaha wa maneno yake na umadhubuti wa hoja zake katika mijadala ya kifiqhi, kiaqida na kisheria, alikua anafanya vikao na wanachuoni wa zama zake ambao walikua wanafunga safari kwa ajili ya kwenda kumuuliza maswali na kujadiliana nae (a.s), kipindi chote cha maisha yake katika mji wa Madina alikua anatoa elimu kwa umma wa kiislamu, na kusimamia mambo mema yaliyo anzishwa na Mtume (s.a.w.w), na kuendelezwa na Imamu Ali kisha Imamu Hassan na Hussein (a.s) halafu baba yake Imamu Ali bun Hussein (a.s).

Imamu Baaqir (a.s) aliishi na babu yake Imamu Hussein (a.s) miaka mitatu na nusu, na alishuhudia mauwaji wa Karbala, kisha akaishi bamoja na baba yake Imamu Sajjaad (a.s) miaka thelathini na nane, kipindi chote hicho alikua anasoma elimu, hekima na utukufu kutoka kwa baba yake, na uongozi wake ulidumu karibu miaka ishirini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: