Alianza kwa kuwakaribisha wageni watukufu, kwa kutaja baadhi ya mashekhe na masayyid walio hudhuria, akawashukuru kwa kuvumilia shida za safari na kuja kwao katika kongamano hili linalo angazia maisha ya Imamu Baaqir (a.s), na mchango wao katika kongamano hili linalo muhusu mtu aliye nyanyaswa na wafalme na bado anaendelea kunyanyaswa hadi sasa kwa kuvunjwa kaburi lake tukufu, amezungumzia nukta nyingi, miongoni mwa nukta hizo ni:
- Jamii inapitia wakati mgumu kuhusu Maimamu wetu (a.s) akiwemo Imamu Baaqir (a.s).
- Watu kuwa mbali na mafundisho ya Mwenyezi Mungu kumeifanya jamii kuwa katika hali mbaya na kuacha baadhi ya ibada muhimu kwa ustawi wa jamii.
- Yatupasa kupambana na upotoshaji wa kuwatambua Maimamu (a.s) hakika wao ni rehma ya Mwenyezi Mungu kwetu.
- Mashekhe zetu na walimu watukufu wanatakiwa kuangalia kwa makini, kwa nini umetokea mmomonyoko mkubwa wa maadili, kama alivyo sema Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi katika khutuba ya Ijumaa, hakika hii ni vita mpya yenye hatari sawa na vita ya Daesh, bali vita hii imekuja kwa sura nyingine, na inalenga zaidi tabaka la vijana.
- Tunatarajia kwenye kongamano hili tutoke na majibu ya hatua za kuchukua katika kupambana na mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu kwa kujifunza mwenendo sahihi wa Maimamu (a.s).
- Kutokana na ushirikiano madhubuti uliopo kati ya hauza na Ataba tukufu, tunatarajia kuwatendea haki maimamu wetu watukufu (a.s) ambao ndio ngao ya kutoangamizwa kwa umma hapa duniani.
- Hakika fatwa tukufu ya kujilinda iliokoa taifa hili lisiangamizwe, baada ya kua ukingoni kabisa mwa kuangamia, iliweza kubadilisha mambo kabisa na kuleta ushindi kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi wa Iraq wazee kwa vijana.