Kusherehekea kumbukumbu ya mazazi matukufu: Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya tano

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir –a.s- ni hazina ya elimu na kilele cha upole), Atabatu Abbasiyya tukufu inaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Baaqir (a.s), kwa kufanya kongamano la tano kwa mwaka wa tano mfululizo, lililo anza asubuhi ya Jumamosi (1 Rajabu 1440h) sawa na (9 Machi 2019m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), likiwa na mahudhurio makubwa yaliyo husisha wageni kutoka sehemu tofauti na viongozi wa kidini na kitamaduni, pamoja na wawakilishi wa Ataba takatifu na mazaru tukufu, wakiongozwa na kiongozi mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai.

Baada ya kusoma Qur’ani ya ufunguzi na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq na kusikiliza wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ulifuata ujumbe wa uongozi mkuu ulio wasilishwa kwa niaba yao na rais wa kitengo cha Dini Shekh Swalahu Karbalai. Kisha ukafuata ujumbe wa wageni ulio wasilishwa na Mheshimiwa Sayyid Muhammad Swadiq Kharsani, miongoni mwa aliyo sema ni: “Bado tunahaja kubwa ya kuchota katika elimu za maasumina (a.s), kwa sababu wao ndio wenye elimu bora inayofaa kuchotwa, mwanaadamu anapo jifunza kwao kila kitu huwa chini yake).

Baada ya hapo mshairi bwana Sajjaad Abdulhamid Mussawi akaburudisha masikio ya wahudhuriaji kwa kusoma tenzi zinazo msifu Imamu Muhammad Baaqir (a.s).

Halafu kikafanyika kikao cha kwanza cha mada za kitafiti kilicho ongozwa na Dokta Sarhani Jafaat, ukasomwa muhtasari wa utafiti usemao: (Miongoni mwa elimu za kifiqhi na mafundisho ya Imamu Baaqir –a.s- mlango wa udhu kama mfano) utafiti wa Ustadh Ali Sa’aduni Alghazi.

Kisha ikatolewa nafasi ya maoni, michango ya mawazo na maswali, na mtafiti alijibu maswali kutoka kwa wahudhuriaji na akasherehesha pale alipo takiwa kusherehesha zaidi, kikao hicho kikafungwa kwa utafiti huo mmoja na kikao kingine kitafanyika Alasiri ya leo ambapo watafiti kadhaa watawasilisha tafiti zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: