Baada ya Adhuhuri ya Jumamosi (1 Rajabu 1440h) sawa na (9 Machi 2019m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanyika kikao cha pili cha uwasilishaji wa mada za kitafiti, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya tano, linalo simamiwa na kufadhiliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir –a.s- ni hazina ya elimu na kilele cha upole), na kuhudhuriwa na watafiti, wasomi wa sekula na watu wa Dini.
Kikao hiki kimeshuhudia usomwaji wa mihtasari mitatu ya tafiti zinazo muhusu Imamu Baaqir (a.s), mihtasari hiyo ilikua kama ifuatavyo:
Utafiti wa kwanza: Umefanywa na Shekh Ali Mujaani kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, anuani ya utafiti inasema: (Imamu Baaqir na mchango wake katika sekta ya Aqida).
Utafiti wa pili: Umefanywa na Dokta Sarhani Jafaat kutoka katika kituo cha Al-Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat, anuani ya utafiti inasema: (Juhudi za islahi zilizo fanywa na Imamu Baaqir (a.s) – Imamu Baaqir muanzilishi wa islahi katika jamii ya waislamu).
Utafiti wa tatu: Umefanywa na Dokta Juma Hamadani kutoka katika chuo kikuu cha Dhiqaar, anuani ya utafiti inasema: (Nafasi ya Imamu Baaqir –a.s- katika kupambana na fikra potofu).
Kikao kilikua na michango mbalimbali kutoka kwa wahudhuriaji pamoja na maswali ambayo watafiti waliyajibu na kufafanua mambo yaliyo lazimika kufafanuliwa zaidi.