Katika kuhitimisha shughuli zake: Washiriki wa kongamano la Imamu Baaqir watoa wito kwa vyuo vikuu na taasisi za utafiti zimuenzi Imamu huyu katika sekta ya siasa, elimu na islahi

Maoni katika picha
Alasiri ya Jumamosi (1 Rajabu 1440h) sawa na (9 Machi 2019m) wamemaliza shughuli za kongamano la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya tano, lililosimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir –a.s- ni hazina ya elimu na kilele cha upole), kwa ajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa nyota ya tano miongoni mwa nyuta za Muhammadiyya Imamu Baaqir (a.s), pamoja na kuangazia maisha yake na utukufu wake, kongamano limepata mahudhurio makubwa ya watu wa kisekula, kitamaduni pamoja na waandishi wa habari.

Hafla iliyo fanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha yakasomwa maazimio yaliyo fikiwa na wana kongamano, yaliyo somwa na mkuu wa Ameed Duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat Dokta Riyaadh Amidi, na maazimio hayo ni:

  • 1- Tunaomba kongamano hili liendelee kufanywa kila mwaka, na libadilishwe kutoka katika kongamano na uwe mkutano wa kimataifa kuhusu Imamu Baaqir (a.s) na mchango wake katika sekta tofauti za maisha.
  • 2- Tunatoa wito kwa vyuo vikuu vya Iraq na taasisi za utafiti zimuenzi Imamu Baaqir (a.s) katika sekta ya siasa, elimu na islahi.
  • 3- Tunatoa wito wa kuchapishwa kwa shughuli za kongamano hili na kuonyesha kua ni endelevu chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya, kutokana na umuhimu wa Imamu huyu katika kila sekta ya maisha ya waislamu.

Hafla ikafungwa kwa kuwapa zawadi washiriki wa kongamano walio wasilisha tafiti na waandishi wa habari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: