Mama yake anaitwa Ummul Waladu, inasemekana jina lake ni Sumana, vilevile huitwa Sumana wa Moroko.
Majina yake ya sifa (laqabu), anamajina mengi, miongoni mwake ni: Murtadhwa, Haadi, Askariy, Aalimu, Dalilu, Muwadhihu, Rashidu, Shahidu, Wafiyyu, Najibu, Mutaqi, Mutawakilu, Khaalisu, Naaswihu, Fataahu, Naqiyyu, Faqiihu, Amiinu, Twayyib, majina maarufu zaidi ni Haadi na Naqiyyu.
Majina yake ya kuniyya, anaitwa: (Abul Hassan) na huitwa Abul hassan wa tatu.
Nafasi yake kielimu (a.s):
Mabingwa wa historia wamekubaliana kua Imamu (a.s) alikua na elimu kubwa sana kushinda wanachuoni wote wa zama zake, Shekh Tusi katika kitabu chake cha (Rijalu Tusi) ameandika majina ya watu mia moja themanini na tano waliosoma na kupokea hadithi kutoka kwake.
Alikua kimbilio la wasomi wa Fiqhi na Sheria, alikua chimbuko la vitabu vya hadithi, mijadala, fiqhi, tafsiri na vinginevyo kutokana na mafundisho yake.
Miongoni wa mafundisho ya Imamu Haadi (a.s):
- 1- Amesema (a.s): “Atakaye ridhia nafsi yake wengi watamchukia”.
- 2- Anasema (a.s): “Msiba wa mwenye subira ni mmoja na asiyekua na subira ni miwili”.
- 3- Anasema (a.s): “Uzembe ni chaguo la wapumbavu na kazi ya wajinga”.
- 4- Anasema (a.s): “Kusinzia ni kutamu kushina kulala na njaa huongeza uzuri wa chakula”.
- 5- Anasema (a.s): “Taja kifo chako kwa familia yako hakuna mganga wala mpenzi atakaekufaa”.
- 6- Anasema (a.s): “Makadirio hukuonyesha usiyotarajia katika akili yako”.
- 7- Anasema (a.s): “Hekima haionekani katika mazingira ya ufisadi”.