Mahaadi ya Qur’ani tukufu ya Atabatu Abbasiyya imechukua majukumu kadhaa yanayo fungamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, kwa lengo la kutambulisha madhumuni yake na kuongeza uwelewa wa Qur’ani, kutokana ma lengo hilo wamekuwa wakifanya harakati mbalimbali, miongoni mwa harakati hizo ni kuendesha vikao vya nadwa ya Qur’ani kila baada ya muda fulani, ikiwemo nadwa hii inayo endeshwa na tawi lake katika wilaya ya Hindiyya yenye anuani isemayo: (Msiihame Qur’ani) mbele ya mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu wa Kadhimiyya Mheshimiwa Shekh Hessein Aali Yaasin.
Nadwa hiyo imefanyiwa ndani ya Husseiniyya ya Qamaru bani Hashim katika wilaya ya Hindiyya na kuhudhuriwa na wasomi wengi wa Qur’ani pamoja na wasomi wa mambo ya kisekula na kundi la waumini, zimezungumzwa mada mbalimbali zinazo husu kuihama Qur’ani, pia umezungumzwa umuhimu wa kudumu katika kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, na kuto kukihama, zikaelezewa hadithi za Mtume na Ahlulbait wake watakasifu (a.s), kisha ikabainishwa maana ya kuihama Qur’ani tukufu na aina zake, ambazo ni: kutoisikiliza na kutoisoma, kutoifanyia kazi, kutoitafakari, kutoifahamu.
Kumbuka kua hii ni miongoni mwa nadwa endelevu za kila mwezi, zinazo andaliwa na tawi la Maahadi tajwa hapo juu, kila mwezi hualikwa wasomi wa Qur’ani kutoka hauza na wasomi wa kisekula kwa lengo la kueneza elimu ya kitabu kitakatifu.