Kumbukumbu inayo umiza: Mwezi tatu Rajabu ni siku aliyo fariki Imamu Ali Haadi (a.s).

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi tatu Rajabu mwaka wa (254h) watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wafuasi wao walipata msiba wa kifo cha Imamu Ali Haadi (a.s), Imamu wa kumi mtakasifu katika Ahlulbaiti Maasumina waliotajwa uongozi wao na Mtume (s.a.w.w).

Imepokewa na Allaamah Majlisiy –r.a- katika kitabu chake cha (Jalaaul-Uyuun) kua: Imamu Ali Haadi (a.s) alikufa kwa kupewa sumu akiwa na umri wa miaka arubaini, na inasemekana alikua na miaka arubaini na moja.

Alishika madaraka rasmi ya Uimamu baada ya baba yake Imamu Jawaad (a.s) akiwa na umri wa miaka sita na miezi mitano, na aliongoza kwa muda wa miaka thelathini na tatu na miezi kadhaa.

Imamu Haadi (a.s) aliishi katika mji wa babu yake Mtume (s.a.w.w) karibu miaka ishirini, kisha Mutawakkil Abbasiy akamtaka aende Samaraa, akaishi huko hadi alipo uwawa kishahidi kwa sumu, na alizikwa ndani ya nyumba yake, sehemu ambapo kaburi yake lipo hadi sasa, baada ya kukaa jela na kizuwizini kwa muda mrefu.

Mtu aliye muua Imamu Haadi (a.s) ni Mu’utamadi Abbasiy, kama ilivyo tajwa na ibun Baabawaihi na wengine, na baadhi ya wanahistoria wanasema aliuliwa na Mu’utazu Abbasiy.

Imamu Haadi (a.s) aliuwawa katika mji wa Samaraa siku tano kabla ya kuisha mwezi wa Jamadal Thani, na inasemekana: aliuwawa mwezi tatu Rajabu, na inasemekana aliuwawa siku ya Jumatatu mwezi ishirini na saba Jamadal Thani mwaka wa (254h).

Masoudi anasema katika kitabu cha (Ithbaatul Waswiyya) Abul Hassan Ali Haadi (a.s) alipo pata maradhi yaliyokua sababu ya kifo chake alikuja mwanae Abu Muhammad na akamuhusia.

Masoudi anasema pia: Alipo fariki (a.s) bani Hashim walikusanyika katika nyumba yake wakiwemo Twalibiyyiina na Abbasiyyiina, pamoja na wafuasi wake wengi, kisha ukafunguliwa mlango wa korido akatoka mfanyakazi mweusi, halafu akatoka Abu Muhammad Hassan Askariy (a.s) akiwa kichwa wazi nguo zimechanika, usowake (a.s) ulikua unafanana sana na uso wa baba yake (a.s), ndani ya nyumba hiyo walikuwemo pia watoto wa Mutawakkil, baada ya kumuona watu woto walisimama.

Akakaa (a.s) katikati ya milango miwili ya korido huku watu wote wakiwa mbele yake, palikua na kelele nyingi kama sokini, lakini baada ya kutoka na kukaa mbele yao watu wote walikaa kimya, hatukusikia ispokua sauti ya chafya na mwayu, kisha mfanya kazi akatoka na akasimama pembeni ya Abu Muhammad (a.s), halafu likatolewa jeneza lake (a.s), Abu Muhammad alikua amesha mswalia kabla hajatolewa mbele za watu, akaswaliwa tena alipo kuja Mu’utamad, kisha akazikwa katika nyumba yake, mji wa Samaraa ulijaa vilio kutokana na kifo chake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: