Maoni katika picha
Majlisi ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha akapanda katika mimbari Shekh Muhsin Asadiy kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, akazungumzia vipengele muhimu vya tabia njema katika maisha ya Imamu wa kumi Ali Haadi (a.s), sambamba na changamoto alizo pambana nazo, alisimama imara kama walivyokua baba zake na babu zake dhidi ya uzushi wowote uliotaka kuingizwa katika uislamu halisi uliofundishwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Akaelezea pia dhulma alizo fanyiwa na watawala wa zama zake na kisa cha kuuwawa kwake, ambapo kifo chake kinafanana na vifo vya babu zake walio uwawa kutokana na chuki ya bani Abbasi dhidi ya kizazi cha Mtume Muhammad (a.s), aliuwawa kwa sumu akiwa ni mwenye kufanya subira mwenye kudhulumiwa.
Majlisi ilihitimishwa kwa kusoma kaswida na tenzi za huzuni zilizo amsha hisia za majonzi kutokana na msiba huu unaoumiza roho za waumini kwa kufiwa na Imamu Ali Haadi (a.s).
Fahamu kua leo siku ya Jumatatu sawa na (3 Rajabu) ni siku ya kukumbuka kifo cha Imamu Ali Haadi (a.s), wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia wanaomboleza msiba huu.