Mbele ya kaburi lake takatifu katika mji wa Samaraa: Pamejaa makundi ya mazuwaru na mawakibu za waombolezaji wanaohuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Haadi (a.s) na Atabatu Abbasiyya inaendeleza juhudi zake za kuimarisha ulinzi na kutoa huduma.

Maoni katika picha
Katika kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Haadi (a.s) Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kila iwezalo kwa ajili ya kuboresha huduma kwa mazuwaru na mawakibu za waombolezaji zilizo kuja katika ardhi hii tukufu kutoka ndani na nje ya Iraq, kwa ajili ya kutoa pole na kuomboleza msiba huu, na kuwawezesha kufanya ibada ya ziara kwa amani na utulivu, pia kuna mawakibu Husseiniyya nyingi zinazo toa huduma ya chakula na vinywaji kwa mazuwaru, pamoja na huduma za kimatibabu na zinginezo.

Vitengo vya Ataba tukufu vilikua vimesha weka mkakati maalumu wa kuhudumia mazuwaru watukufu, kitengo cha wageni chiniya uongozi mkuu wa Atabatu Askariyya tukufu kimetangaza kutoa huduma ya chakula kupitia mgahawa wa Maimamu wawili Askariyyaini (a.s), wanagawa chakula muda wote hadi usiku wa manane, kwa kushirikiana na mawakibu za Ataba zingine pamoja na mawakibu za watoa huduma.

Kamati ya mawakibu imetangaza sehemu maalumu za mawakibu zinazo toa huduma kwa mazuwaru, ambapo zipo katika njia zinazo tumiwa na mazuwaru, kituo cha madaktari pia kimetangaza uwepo wa huduma za matibabu katika hema za kitabibu zilizo wekwa njiani pamoja na kwenye gari za wagonjwa.

Kitengo cha Dini kwa kushirikiana na kamati ya mawakibu pamoja na kitengo cha mahusiano wameweka utaratibu wa upokeaji wa mawakibu za waombolezaji na kuwarahisishia shuguli za uombolezaji wao ndani ya haram tukufu, pia wanasimamia swala za jamaa ndani ya haram tukufu pamoja na kwenye korido za Imamu Haadi na kwenye Sardabu ya ghaiba na kwenye lango kuu la kuingia pamoja na kwenye haram ya bibi Narjis, hali kadhalika vituo vya maswali na majibu vimekua na nafasi kubwa kupitia mubalighina, Masayyid na Mashekh waliokuja kutoka mikoa tofauti, vilevile kulikua na vituo vya usomaji wa Qur’ani pamoja na ufundishaji wa kusoma kwa usahihi surat Fat-ha na zinginezo.

Kitengo cha kulinda nidhamu kimesimamia vizuri misafara ya watembeaji kuanzia sehemu wanazo shuka kwenye magari hadi kwenye malalo takatifu, kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi na usalama.

Kitengo cha habari kimeandaa kadi maalumu kinazo toa kwa waandishi wa habari wanaokuja pamoja na misafara ya waombolezaji au mawakibu, sambamba na matangazo ya moja kwa moja (mubashara) yanayo endelea kuonyesha mawakibu za waombolezaji na mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: