Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni katika utaratibu wake maalumu katika kuomboleza vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), imegawa mamia ya sahani za chakula kwa mazuwaru waliokuja katika mji wa Karbala kuomboleza kifo cha Imamu Ali Haadi (a.s), kwa kutumia madirisha ya kugawa chakula ya nje.
Fahamu kua makundi makubwa ya waumini –pamoja na mawakibu za waombolezaji- kutoka Karbala na miji jirani, katika siku kama ya leo huja kwenye kaburi la Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake mbeba bendera wake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Ali Haadi (a.s).