Atabatu Abbasiyya tukufu imepandisha bendera za huzuni na inapokea mawakibu za waombolezaji katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Ali Haadi (a.s).

Maoni katika picha
Huzuni imetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuta zake zimewekwa mapambo meusi na imetangaza maombolezo ya kukumbuka kifo cha Imamu Haadi (a.s), bendera za maombolezo zimepandishwa, na vitambaa vilivyo andikwa maneno yanayo ashiria huzuni vimewekwa ndani ya haram tukufu kama sehemu ya kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu kama desturi yake imeandaa ratiba ya kuomboleza yenye vipengele vingi, kuna utowaji wa mihadhara ya kidini, na vikao (majlisi) za kuomboleza.

Kwa upande mwingine kama walivyo zowea kufanya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kukumbuka msiba miongoni mwa misiba ya watu wa familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), asubuhi ya leo (3 Rajabu 1440h) sawa na (11 Machi 2019m) yamefanyika matembezi maalumu ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali Haadi (a.s), yakielekea katika kaburi la bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoa pole kwao na kwa Imamu Hujjat msubiriwa (a.f) kutokana na msiba huu mkubwa.

Matembezi ya waombolezaji yalianzia katika barabara zinazo elekea kwenye malalo ya mnyweshaji wenye kiu Karbala (Saaqi Atwaasha Karbala) (a.s), waliimba kaswida na kusoma tenzi zilizo onyesha ukubwa wa huzuni waliyo nayo katika roho zao, kisha wakaelekea kwa Imamu Hussein (a.s) kuzuru kaburi lake takatifu wakipitia katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakipiga matam na kuimba, baada ya kuwasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s) walifanya majlisi karibu na kaburi la baba wa maimamu (a.s).

Kuhusu uingiaji wa mawakibu hizo ndani ya haram ya Abbasi (a.s) na utokaji wao, tumeongea na rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyaadh Ni’imah Salmaan ambaye amesema kua: “Kitengo chetu katika matukio kama haya huandaa ratiba ya uingiaji na utokaji wa mawakibu za ndani na nje ya mkoa wa Karbala, baada ya kupokea maombi ya mawakibu zinazo taka kushiriki katika maombolezo hayo, kisha kila maukibu hupewa muda wa kuingia na kutoka pamoja na mahala wanapo takiwa kuanzia kutembea na mahala wanapotakiwa kuishia, kwa ajili ya kudhibiti mpangilio wa matembezi yao na kuhakikisha hayakwamishi harakati za mazuwaru, kila maukibu husindikizwa na watumishi wa kitengo chetu kwa ajili ya kusaidia uwekaji wa nidhamu za matembezi, leo katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Haadi (a.s) tumepokea makumi ya mawakibu za waombolezaji zilizo anza kuwasili tangu asubuhi hadi jioni.

Mji mtukufu wa Karbala umejaa majonzi na huzuni, kutokana na msiba huu unaoumiza roho za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Kumbuka kua Ataba tukufu za Karbala pia hufanya matembezi maalumu ya kuomboleza vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika kipindi chote cha mwaka, na huanzia mbele ya Atabatu Husseiniyya tukufu hadi kwenye Atabatu Abbasiyya au kinyume chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: