Maoni katika picha
Yametokea hayo katika ziara iliyo fanywa na ugeni huo na kuongozwa na Profesa CIGDEM MAER kutoka chuo kikuu cha Bolina Italia na chuo kikuu cha Kotesh cha Istambul Uturuki, wametembelea makumbusho hiyo huku wakisindikizwa na rais wa makumbusho Ustadh Swadiq Laazim, wageni wasikiliza maelezo kwa ufupi kuhusu makumbusho na njia ya uhifadhi wa vifaa vyake, pia wametembelea ukumbi wa maonyesho ya vifaa vilivyopo katika makumbusho, pamoja na kupewa maelezo kwa kifupi kuhusu kila kifaa.
Mwishoni mwa ziara yao Pr. CIGDEM MANER Alionyesha kuridhiswa kwake na alicho kiona katika makumbusho hiyo, akasema: “Nawapongeza sana kutokana na makumbusho hii ya kimataifa” akasisitiza kua: “Hakika hii ni makumbusho kubwa na inavitu vingi vya thamani”.
Baada ya hapo ugeni ulikwenda kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi, wakajadili mambo mbalimbali kuhusu uzowefu wao katika mambo ya makumbusho na kuhusu wanafunzi wa Alkafeel wanao somea mambo ya makumbusho.