Zaidi ya wanajeshi (300) wa kikosi cha Abbasi wamemaliza kazi yao ya ulinzi na kutoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Haadi (a.s).

Maoni katika picha
Zaidi ya wanajeshi (300) wa kikosi cha Abbasi (a.s) wamemaliza jukumu lao la kuimarisha ulinzi na kutoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Haadi (a.s) katika mji mtukufu wa Samaraa, wametekeleza majukumu yao kwa kushirikiana na Atabatu Askariyya pamoja na vikosi vingine vya ulinzi na usalama.

Sayyid Hashim Mussawi ambaye ni rais wa kitengo cha mahusiano wa kikosi cha Abbasi (a.s) na kiongozi wa maukibu ya kutoa huduma katika mji wa Samaraa amesema kua: “Vitengo vya kikosi cha Abbasi (a.s), kikiwemo kitengo cha mahusiano, ulinzi na uhandisi vimeshiriki kikamilifu katika kuimarisha ulinzi na utowaji wa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Haadi (a.s) kwa Zaidi ya siku tatu mfululizo”.

Akaongeza kua: “Katika program hii wameshiriki Zaidi ya wanajeshi (300) wa kujitolea ambao wako chini ya kikosi cha Abbasi (a.s) sambamba na wanajeshi wa hakiba waliosaidia ukaguzi katika njia zinazo tumiwa na mazuwaru kuelekea Atabatu Askariyya tukufu kwa lengo la kuimarisha amani na usalama”.

Akasisitiza kua: “Maukibu ya kutoa huduma imegawa chakula na maji kwa mazuwaru watukufu, pamoja na kufanya kazi zingine, kama vile kufanya usafi katika njia zinazo elekea Atabatu Askariyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: