Katika mradi wa vituo vya Quráni: Maahadi ya Quráni tukufu imetangaza mafanikio yake katika kuwafundisha mazuwaru wa Maimamu wawili Askariyyaini (a.s) usomaji sahihi.

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufanikiwa kwa mpango wake wa kufundisha usomaji sahihi wa Quráni kwa mazuwaru wa Maimamu wawili Askariyyaini (a.s), walioutekeleza kwa kushirikiana na Atabatu Askariyya tukufu, kwa kuweka vituo kadhaa katika barabara zinazo elekea kwenye malalo takatifu, na kunufaika na makundi makubwa ya waumini wanao kwenda kufanya ziara.

Vituo hivyo vilidumu kwa muda wa siku tatu mfululizo, na vilikua na makumi ya walimu waliokuwa wanasikiliza usomaji wa zaairu kasha wanamrekebisha kama akiwa na makosa katika usomaji wake, vituo hivyo vimepata mwitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru hususan wa mataifa yasiyo kua ya kiarabu, mazuwaru wamesifu na kushukuru uwepo wa mradi huu unao waonyesha umuhimu wa kujifundisha usomaji sahihi wa Quráni ambayo ni sharti la kuswihi kwa swala.

Vituo hivyo vilikua na majukumu mengi, miongoni mwa majukumu hayo ni:

  • 1- Kufundisha usomaji sahihi wa aya za Quráni hususan zinazo somwa katika faradhi ya swala.
  • 2- Kujibu maswali yanayo husu Quráni.
  • 3- Kuendesha visomo vya Quráni tukufu kulingana na kila sehemu kilipo kituo.
  • 4- Kugawa vipeperushi vinavyo elezea ziara na mambo yanayo husu Quráni.

Pia Maahadi imeendesha usomaji wa Quráni katika mji wa Samaraa kwa ushiriki wa jopo kubwa la wasomaji, na kuhudhuriwa na mazuwaru wengi waliokaa na kusikiliza Quráni takatifu ndani ya eneo hilo tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: