Rais wa Iran atembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Adhuhuri ya leo (4 Rajabu 1440h) sawa na (12 Machi 2018m) Rais wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran Shekh Hassan Rohani ametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) akisindikizwa na mkuu wa mkoa wa Karbala Ustadh Aqiil Twarihi.

Alipo wasili katika malalo takatifu alipokelewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqari pamoja na jopo la viongozi wa kamati kuu, kisha akaenda kufanya ziara katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kuswali.

Baada ya hapo akaagwa kwa kwa furaha kama alivyo karibishwa na hiyo ndio kawaida ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kupokea wageni wa aina zote bila kujali madaraka yao.

Baada ya kulamiza ziara, Rais wa Iran amewashukuru wasimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na maendeleo ya kuijenzi aliyo yaona ndani na nje ya malalo tukufu, akawaombea taufiq na kuendelea na kazi yao, kisha akaenda kumzuru bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: