Kutoka Najafu Ashrafu: Kuanza kwa kongamano la kimataifa kuhusu lugha ya kiarabu baina ya asili na uboreshwaji

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo (Hauza ni kitovu cha mabadiliko) ukiwa ni mwendelezo wa awamu tatu zilizo pita, Alasiri ya leo Jumatano (5 Rajabu 1440h) sawa na (13 Machi 2019m) limeanza kongamano la nne la kimataifa kuhusu lugha ya kiarabu na fani zake baina ya asili na maboresho, linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na taasisi ya Bahrul-Uluum Alkhairiyya, linalo fanyika katika mkoa wa Najafu na kuhudhuriwa kwa wingi na viongozi mbalimbali pamoja na wageni kutoka taasisi za elimu ya dini na sekula ndani na nje ya Iraq, pambaja na wajafunzi wa hauza na wadau mbalimbali wa lugha ya kiarabu, miongoni mwao ni katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu Sayyid Jafari Mussawi pamoja na katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya Dokta Jamali Dabaagh, sambamba na ugeni mkubwa kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu ukiongozwa na kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), pamoja na vyombo vya habari kwa ajili ya kutangaza matukio ya kongamano hili.

Kongamano litakua la siku tatu, lilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu na kufuatiwa na mada mbalimbali zitakazo andikwa katika mtandao wa kimataifa Alkafeel hapo baadae.

Kumbuka kua kongamano linalenga kuangalia matokeo ya tafiti za kilugha, na kubaini hazina iliyo nayo kitamaduni, kijamii na kisiasa, na nafasi ya hauza katika kuhuisha elimu za lugha ya kiarabu za fani zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: