Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Wanalugha ya kiarabu wanahaja ya kujua nafasi yake na nguvu yao inatokana na nguvu ya lugha yao…

Maoni katika picha
Katika kongamano la nne la kimataifa kuhusu lugha ya kiarabu na fani zake baina ya asili na uboreshwaji, linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na taasisi ya Baharul- Ulumi Alkhairiyya, lililo anza baada ya Ahduhuri ya siku ya Jumatano (5 Rajabu 1440h) sawa na (13 Machi 2019m) katika mji wa Najafu chini ya kauli mbiu isemayo: (Hauza ni kitovu cha mabadiliko), kulikua na ujumbe kutoka kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na mjumbe wa kamati ya uongozi Dokta Abbasi Didah, ifuatayo ni nakala ya ujumbe huo:

Sisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu tunaona kua lugha ya kiarabu ni kitu kikubwa kwa heshima ya mwanaadamu, pia ni nguzo ya utambulisho wake na njia kuu ya kueleza haja yake na kutambua uwezo wake wa kiakili.

Mshairi anasema:

Nimeona lugha ya mtu ni mgeni wa akili wake*** na ndio anuani yake angalia ana anuani gani.

Hii ni kwa lugha zote, vipi lugha ambayo imetuletea mafundisho ya kiislamu, na ndio ufunguo wa elimu zake na mbeleko (bebeo) ya utamaduni wake, vipi kiarabu kilicho chaguliwa na Mola mtukufu kua lugha ya maneno yake, na akapanga itumike kuandika maneno ambayo ni muujiza na yatunzwe kwa lugha hii ya kiarabu.

Bila shaka lugha ya kiarabu ni ya kudumu milele na milele katika lugha za walimwengu, hakuna shaka pia kua inasifa za pekee zilizo ifanya ipate nafasi hiyo, sio kwa sababu tu waarabu ni waislamu, bali lugha hii ni tukufu hata kwa wasiokua waarabu, kuna mfaransa mustashrik (asiyekua mwislamu) bwana Richi Blashir anasema: “Hakika miongoni mwa upekee wa lugha ya kiarabu ni uwezo wa maneno yake kua na maana ya pili ambayo watu wa magharibi hawawezi kuielezea”.

Inawezekana watu wake leo na katika kila siku wanahaja ya kutambua maneno yake na hadhi yake pamoja na utukufu wake, bila shaka utukufu wao unatokana na utukufu wa lugha yao, hapo zamani hakimu aliulizwa: Utafanya nini ukipewa uongozi wa taifa hili? Akasema: Jambo la kwanza nitarekebisha lugha, kwani kurekebisha lugha kunaleta mawasiliano sahihi na lugha ndio utambulisho wao na msingi wa uwepo wao.

Enyi ndugu! Kiarabu kuingizwa rasmi na umoja wa mataifa mwaka (1973m) katika lugha za kimataifa sio bahati mbaya, ni kutokana na utukufu wake ulio onekana wazi katika idara ya kimataifa, lugha hii inahaki ya kudumu iliyo pewa na uislamu mtukufu, ni lugha isiyokua na mipaka ya kijografia, kwani ni lugha ya uislamu ulio eneo kila sehemu ya dunia.

Hakika uasili tunaokusudia ni wa kulinda lahaja katika uhalisia wake, na uboreshaji ni kufuata misingi ya lugha na fani zake ambazo ni nyingi kupita kifani.

Kwa kua lazima kuwepo na urahisishaji wa kujifunza na kuielewa, linapo tokea tatizo sio la lugha, bali litakua tatizo la kutoifanyia kazi lugha.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awarehemu wanachuoni watukufu walio tangulia, na awape muri mrefu waliopo wenye neema na baraka, awape nguvu wasimamizi wa kongamano hili na awajaalie waweze kuendeleza mazuri waliyo anzisha, na awawafikishe watafiti na washiriki wote kwa ujumla hakika yeye peke yake ndio mkuu wa kuwafikisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: