Usiku wa Raghaaibu: Ni usiku wa Ijumaa ya kwanza katika mwezi wa Rajabu.. maana yake, utukufu wake na ibada zake.

Maoni katika picha
Imezungumzwa mara nyingi kuhusu ibada zinazo takiwa kufanywa katika mwezi wa Rajabu, miongoni mwake ni usiku wa Ijumaa ya kwanza katika mwezi wa Rajabu, ambao huitwa usiku wa Raghaaibu, Mtume (s.a.w.w) anasema: (Msighafirike katika usiku wa Ijumaa ya kwanza –katika mwezi wa Rajabu- hakika usiku huo Malaika wanauita kua ni usiku wa Raghaaibu, inapofika theluthi ya usiku malaika wote wa mbinguni na ardhini hukusanyika katika Kaaba tukufu, kisha Mwenyezi Mungu huwaangalia na kuwaambia: Enyi malaika wangu niombezi mtakacho, husema: Ewe Mola wetu tunakuomba uwasamehe wanaofunga katika mwezi wa Rajabu, Mwenyezi Mungu huwajibu: nimekwisha wasamehe).

Usiku wa Raghaaibu maana yake ni, usiku wa kutoa sana, usiku huu unautukufu mkubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, humlipa thawabu nyingi sana mwenye kufunga mchana wake na kuhuisha usiku wake kwa kufanya ibada na vitendo vyema, katika usiku huu waliofunga na wanaofanya istighfaar huwasilisha maombi yao, na Mwenyezi Mungu huwapa wanayo yataka, ndio maana Malaika wakauita usiku huu kuwa ni usiku wa Raghaaibu (kupewa unacho kitaka).

Usiku wa Raghaaibu una ibada maalumu, Mtume (s.a.w.w) anasema: (Yeyote atakayefunga siku ya Alkhamisi ya kwanza katika mwezi wa Rajabu kisha akaswali baada ya Isha rakaa kumi na mbili, kisha aniswalie mara sabini, halafu aseme, Subuuhu Quduusu Rabbu, mara moja, kisha aseme: Allahumma Swali alaa Muhammad wa alaa Aalihi, kisha asujudu na aseme katika sajda yake, Malaaikatu wa Ruuhu, mara sabini, kisha ainue kuchwa chake kutoka kwenye sijda na aseme: Rabbi-ghfir warham watajaawaz ammaa ta’alam innaka anta Al-aliyul-adhiim, kisha asujudu mara ya pili na asome kama alivyo soma mara ya kwanza, kisha aombe haja zake kwa Mwenyezi Mungu akiwa kwenye saijda, hakika atakidhiwa).

Kisha Mtume (s.a.w.w) akasema: (Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo ndani ya uwezo wake, yeyote atakaye swali swala hii atasamehewa dhambi zake zote hata kama zikiwa kama povu la baharini, na atapewa nafasi ya kuwaombea shifaa siku ya kiyama watu mia saba waliokuwa wamehukumiwa moto katika familia yake).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: