Kutoka katika mji wa Imamu Ali (a.s): Kikao cha usomaji wa mashairi kilicho kumbusha nafasi ya mashairi kihistoria

Ukumbi wa Shekh Tusu katika taasisi ya Bahrul Uluum Alkhairiyya huko Najafu, ikiwa ni miongoni mwa program za kongamano la kimataifa kuhusu lugha ya kiarabu linalo simamiwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, wamefanya kikao cha usomaji wa mashairi na kushiriki wasomaji kutoka ndani na nje ya Najafu, washairi walithibitisha umuhimu wa mashairi kihistoria na wakaonyesha kua mkoa wa Najafu unamchango mkubwa katika fani ya mashairi.

Kisomo hiki kinafanywa kwa mara ya kwanza katika kongamano la kimataifa liitwalo (Hauza ni kitovu cha mabadiliko), ratiba hii imeingizwa katika kongamano hili kutokana na umuhimu mkubwa wa mashairi katika lugha ya kiarabu, kikao hiki kimehudhuriwa na viongozi wengi wa dini na wasomi wa lugha kutoka ndani na nje ya mkoa wa Najafu, walio shiriki katika kusoma mashairi ni:




    • 1- Sayyid Muhyi Jaabiri.




    • 2- Ustadh Hussein Qaaswidi.




    • 3- Thaamir Assaaf.




    • 4- Swadiq Gharifi.




    • 5- Najaah Arsaani.




    • 6- Ibrahim Naswirawi.




    • 7- Masaar Yaasiriy.




    • 8- Yaasi Saidi.




    • 9- Ridwa Sayyid Jafari.




    • 10- Mahadi Nahiri.




    • 11- Qassim Tamimi.




Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hili na katibu mkuu wa taasisi ya Bahrul Uluum Alkhairiyya, Sayyid Muhammad Ali Bahrul Uluum ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ni jambo zuri sana kongamano letu kuwa na kikao cha usomaji wa mashairi, tena kwa kuzingatia aina za fani zilizo kuwa mashuhuri zaidi katika mji wa Imamu Ali (a.s) ambayo ni fani ya mashairi, ilikua na bado inaendelea kutoa Marjaa na watu wa dini, walimu na washairi, miongoni mwa sifa kubwa ya fani hii hata msomi wa dini huwa ni mtaalamu wa mashairi na fani za lugha ya kiarabu, daima mashairi huenda sambamba na fani mbalimbali, kutokana na ukweli huo tukaona ni vizuri kuwa na kikao cha usomaji wa mashairi katika kongamano hili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: