Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika wiki ya kilimo na siku ya mti

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika wiki ya kilimo na siku ya mti hapa Iraq, inayo simamiwa na wizara ya kilimo chini ya kauli mbiu isemayo: (Tuifanye Iraq kua kijani kibichi) kuanzia tarehe (14-21 Machi 2019m) katika uwanja wa maonyesho wa Bagdad.

Atabatu Abbasiyya tukufu imekua ikishiriki katika maonyesho na makongamano mbalimbali ya ndani na nje ya Iraq, ya kitaifa na kimataifa, katika maonyesho haya Ataba tukufu imewakilishwa na:

  • Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa na viwanda Aljuud, ambalo linaonyesha aina tofauti za mbolea wanazo tengeneza, pamoja na dawa mbalimbali ambazo ni rafiki kwa mazingira na zenye mchango mkubwa katika kuboresha kilimo na kukiendeleza.
  • Shirika ya uchumi Alkafeel, ambalo linaonyesha:
  • 1- Mazao kutoka katika mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile matango, bilinganya, nyanya na mengineyo, mazao yenye ubora mkubwa, sifa yake kubwa ni kwamba yanalimwa kisasa tena bila kutumia kemikali, jambo linalo yafanya kuchukua nafasi ya kwanza ya ubora katika soko la Iraq.
  • 2- Kiwanda cha Alwaahah cha kutengeneza chakula cha kuku, wanaonyesha malighafi muhimu wanazo tegemea.
  • 3- Mashamba ya kuku, wanaonyesha uzowefu wao katika ufugaji.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa matawi yanayo shiriki katika maonyesho haya, ushiriki wao unatokana na maelekezo ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya kilimo katika taifa letu, pia kushiriki katika maonyesho haya ni fursa kubwa ya kuwasiliana na sekta za nje pamoja na kutambua maendeleo yaliyopo kwa wengine katika sekta hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: