Mradi wa mimbari za Nuru unaendelea kufanya hafla za usomaji wa Quráni na wilaya ya Afku ni moja ya vituo vyake

Maoni katika picha
Miongoni mwa miradi ya Quráni endelevu ni mradi wa mimbari za nuru, unaohusisha kufanya mahafali za usomaji wa Quráni ndani na nje ya mkoa wa Karbala, na katika Ataba tukufu au Mazaru takatifu, na ndani ya husseiniyya na misikiti, na kwa kushiriki wasomaji wa Quráni kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, chini ya utaratibu maalumu unaolenga kuimarisha utamaduni wa kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kuchangia katika kufanya harakati za usomaji wa Quráni.

Wilaya ya Afku iliyopo kaskazini ya mkoa wa Diwaniyya ilikua moja ya vituo vya mradi huo, kimefanyika kikao cha usomaji wa Quráni katika mji huo unaopenda Quráni kwa kushirikiana na Darul Quráni, ambapo kitabu cha Mwenyezi Mungu kimesomwa kwa mahadhi na sauti nzuri, wameshiriki wasomaji kadhaa wakiwemo wa Ataba mbili tukufu Sayyid Hussein Halo na msomaji wa Atabatu Abbasiyya Liith Ubaidiy na msomaji wa Darul Quráni tukufu katika wilaya hiyo bwana Murtadha Hussein, na mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa Mauhubu Khaliil Twaha.

Mahafali ilikua na mazingira mazuri ya kiimani na ilipata mwitikio mkubwa kutoka kwa waumini na wadau wa Quráni tukufu, walio fika kusikiliza Quráni tukufu iliyo kua inasomwa kwa mahadhi mazuri na sauti murua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: