Kituo cha ukarabati wa nakala kale kinaangalia namna ya kushirikiana na kituoa cha kitaifa cha kutunza jinai za chama cha Baáth na taasisi ya Shuhadaa na uongozi wa shuhuda za jinai.

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kuimarisha uhusiano baina ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na taasisi zingine za serikali na zakiraia zinazo fanana nayo, kwa lengo la kubadilishana uzowefu na mambo yanayo wajumuisha.

Wajumbe wa kituo cha kurekebisha nakala kale wametembelea kituo cha kitaifa cha kutunza kumbukumbu za jinai zilizofanywa na chama cha Baáth pamoja na kuitembelea taasisi ya shuhuda za kijinai kwenye kitengo chake cha nakala kale (makhtutwaat), kupitia ziara hii wamekubaliana mambo kadhaa yanayo husu kufanya kazi kwa kushirikiana baina yao, na namna ya kunufaika na uzowefu wa pande zote mbili, na namna ya kuwa na mwelekeo sahihi kwa faida ya pande zote mbili, baada ya kumaliza ziara hiyo, ujumbe wa wageni uliwapa zawadi wenyeji wao kutokana na ushiriki wao katika siku ya nakala kale za kiarabu.

Wageni hao walipokelewa na makamo kiongozi mkuu wa kituo cha kitaifa cha kutunza jinai cha chama cha Baáth na mkuu wa kitengo cha nakala kale Ustadh Muhammad Abdukaatwii pamoja na Omari Saaidiy kutoka ofisi ya shuhuda za kijinai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: