Mwezi tisa Rajabu ni kumbukumbu ya kuzaliwa Ali Asghar –Abdullahi Radhwii- (a.s).

Maoni katika picha
Imepokewa kuwa mwezi tisa Rajabu mwaka (60h) Imamu Hussein (a.s) alipata mototo aliye nawirisha mji wa Madina kwa kuzaliwa kwake, Mwenyezi Mungu mtukufu alimtunuku mototo aliye jaza shangwe na furaha kwa mjukuu wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), Mwenyezi Mungu mtukufu alimpatia mototo ambaye waumini walikua wanatawasali kwake katika kuomba haja zao kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Baba yake ni: Imamu Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s) mjukuu wa Mtume (s.a.w.w).

Mama yake ni: Rubaab bint Imri Qaisi bun Adi –mshairi maarufu-.

Kupewa jina kwake baada ya kuzaliwa: Baada ya kuzaliwa kwake (a.s) Imamu Hussein (a.s) alimpa jina la watoto wake wengine, jina la Ali Asghar, kama alivyo waita wototo wake wawili kabla yake Ali Akbar na Ali Sajjaad (a.s), alisema: (Lau Allah angemruzuku wavulana elfu moja angewaita Ali kutokana na mapenzi aliyokua nayo kwa baba yake mtu wa kwanza kudhulimiwa hapa duniani Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).

Abdullahi Radhii ni askari mdogo zaidi katika watu walio mnusuru Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala na walii mkubwa zaidi katika mawalii wa Mwenyezi Mungu vilevile ni mlango miongoni mwa milango ya kuomba haja kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, pia ni madhulumu mkubwa mno katika historia, aliuwawa akiwa na miezi sita tena akiwa na kiu kwa mkuki ulio tiwa sumu na wenye ncha tatu, aliorushiwa na Maluuni Harmala bun Kaahil Asadiy kutoka katika mji wa Kufa, mkuki huo ukamchinja akiwa mikononi mwa baba yake katika vita ya Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: