Waziri mkuu wa Iraq asifu mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya kilimo.

Maoni katika picha
Waziri mkuu wa Iraq Dokta Aadil Abdul-Mahdi amesifu mafanikio ya Atabatu Abbasiyya katika sekta ya kilimo na bidhaa zinazo zalishwa na Ataba tukufu, ameonyesha kufurahishwa kwake na mafanikio hayo na akatoa wito wa kuendelea kuboresha zaidi sekta hii muhimu kwa uchumi wa taifa.

Ameyasema hayo alipo tembelea matawi la Atabatu Abbasiyya tukufu yanayo shiriki kwenye maonyesho ya wiki ya kilimo na siku ya miti, yanayo fanyika kwa mara ya kumi na moja hapa Iraq, na kusimamiwa na wizara ya kilimo chini ya kauli mbiu isemayo: (Tuifanye Iraq kua ya kijani kibichi) katika uwanja wa maonyesho ya kimataifa wa Bagdad, baada ya kutembelea matawi hayo alisikiliza maelezo kutoka kwa kiongozi mtendani wa shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa na bidhaa za viwandani Aljuud, Mhandisi Maitham Ali Hussein Bahadeli.

Kumbuka kua mashirika yanayo iwakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho haya ni: Shirika la teknolojia ya kisasa na vifaa vya viwandani Aljuud, mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s), Kiwanda cha Waahah kinacho tengeneza chakula cha kuku, kiwanda cha kutotolea mayai ya kuku, ambao wanaeleza mipango ya Atabatu Abbasiyya tukufu na bidhaa wanazo tengeneza, zinazo saidia kujenga taifa kwa kiwango kinacho endana na maendeleo ya zama hizi, pia ni fursa ya kuangalia maendeleo ya kisasa yaliyopo katika taasisi zingine katika sekta ya kilimo, sambamba na kubadilishana uzowefu katika mambo ya kilimo kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: