Mwezi kumi Rajabu ardhi iliangaziwa na nuru ya Imamu Jawaad (a.s).

Maoni katika picha
Mwezi kumi Rajabu ni kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Muhammad Jawaad ambaye ni Imamu wa tisa miongoni mwa maimamu wa Ahlulbait (a.s), jina lake kamili ni Muhammad bun Ali bun Mussa bun Jafari bun Muhammad Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s).

Alizaliwa mwezi kumi Rajabu mwaka wa (195h), uso wa baba yake Imamu Ridhwa (a.s) ukajaa furaha kwa kuzaliwa kwake, baada ya kuzaliwa tu alisujudu na kushuhudia kua Mwenyezi Mungu ni mmoja na Muhammad (s.a.w.w) ni mjumbe wake.

Imamu Ridwaa (a.s) alikua amesha muambia dada yake akae pembezoni mwa mke wake Khazirani (mama wa Imamu Jawaad) baada ya kuonekana dalili za uchungu.

Bi Hakima dada wa Imamu Ridwaa (a.s) alishangaa kuona nuru kubwa inaangaza, na kuzaliwa kwa mtoto akiwa amesujudu, lakini hiyo ilikua ndio kawaida ya Maimamu watakasifu walio teumiwa na Mwenyezi Mungu kuwa hoja kwa walimwengu, wao sio kama baadhi ya viumbe katika mienendo yao, hata wanapokua katika matumbo ya mama zao, wala sio ajabu Imamu Kuzaliwa na kusujudu kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kutamka shahada mbili, yote hayo ni kuthibitisha uimamu wake kwa walimwengu.

Imamu Jawaad (a.s) alikua na maajabu mengi katika umma wa kiislamu, alichukua nafasi ya Uimamu Baada ya baba yake Imamu Ridhwaa (a.s) akiwa na umri wa miaka tisa, ni jambo ambalo liliwashangaza hadi baadhi ya wafuasi wa Imamu Ridwaa (a.s), Imamu alipo ulizwa nani atachukua nafasi yake akamuashiria wakati akiwa bado na umri mdogo, ndio! Walitambua kupitia habari ya Issa mwana wa Maryam na habari za Yahya bun Zakariya (a.s) tangu zamani, Qur’ani tukufu imehadithia visa vyao, lakini ni jambo la kawaida kwa mwanaadamu kuangalia zaidi ushahidi wa vitu, na mazowea, wakati inatakiwa wanapo ona miujiza ya Mwenyezi Mungu wasiwe na chaguo lingine zaidi ya kusalim amri.

Hiyo ndio ilikua tofauti ya Imamu Jawaad (a.s) na Maimamu wengine watakasifu, alichelewa kuzaliwa hadi wafuasi wa Ahlulbait wakakosa amani, kisha alishika madaraka ya Uimamu akiwa na umri mdogo na mwenye akili kubwa, alikua sio wa kawaida katika maneno, hekima na elimu yake, halafu aliuwawa akiwa bado kijana mdogo asiye zidi miaka ishirini na tano.

Pamoja kua mwanaye Imamu Ali Haadi (a.s), pia alishika madaraka akiwa na umri mdogo, lakini habari za uongozi wa Imamu Ali Haadi (a.s) zilisambaa akiwa bado ana umri mdogo, kwa sababu sehemu ya kumtangaza ilikua ni katika Qasri la khalifa Ma-amun aliye andaa mjadala mkubwa kati ya Imamu Jawaad (a.s) na Qadhi mkuu wa kipindi hicho Yahya bun Aktham.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: