Idara ya ustawi wa jamii inakutana na wawakilishi wake wa mikoani na kusisitiza kua mwelekeo wake ujao ni mkoa wa Muthana.

Maoni katika picha
Katika utaratibu wake wa kufanya vikao kila baada ya muda fulani kwa kufuata ratiba maalumu, idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kikao kilicho hudhuriwa na wawakilishi wake wote kutoka mikoani, kwa ajili ya kujadili na kuangalia huduma walizo toa kipindi kilicho pita, ikiwa ni pamoja na misaada waliyo wapa wapiganaji wa serikali na wale wa Hashdi Sha’abi, na misaada mingine ya kibinaadamu.

Mkutano huo umeongozwa na Shekh Abbasi Akaishi, umejadili mpango kazi wa vituo vya ustawi wa jamii katika kipindi kijacho, pia mkutano umepongeza kazi nzuri iliyo yanywa na vituo vya ustawi wa jamii katika mikoa yote pamoja na mawakibu za kutoa huduma zilizo chini yao, halafu wakajadili maandalizi ya kuusaidia mkoa wa Muthanna (Samawah), ikiwa ni ratiba ya Hilla ya kusaidia familia masikini na zile za mashahidi na majeruhi.

Kumbuka kua idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ni moja ya idara muhimu, na imechukua jukumu la kutoa misaada ya kibinaadamu kwenye mikoa yote ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: