Waziri wa kilimo wa Iraq Dokta Swaaleh Hussein Jabri Alhassaniy amepongeza kazi inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya kilimo hapa nchini, na juhudi zake za kuongeza uzalishaji wa ndani kwa kufanya miradi mingi ya kiuchumi.
Ameyasema hayo alipo tembelea matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yanayo shiriki katika maonyesho ya wiki ya kilimo ya kumi na moja na siku ya mti, yanayo simamiwa na wizara ya kilimo chini ya kauli mbiu isemayo: (Tuifanye Iraq kuwa ya kijani kibichi) katika uwanja wa maonyesho ya kimataifa uliopo Bagdad, amesikiliza maolezo kuhusu bidhaa zinazo tengenezwa na Ataba tukufu kutoka kwa kiongozi mtendaji wa shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa na vifaa vya viwandani Aljuud Mhandisi Maitham Hussein Bahadeli.
Akabainisha kua: “Tunaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushiriki katika maonyesho ya wiki ya kilimo, tutajitahiki kuisaidia kwa kuiondolea vikwazo vyote vinavyo weza kukwamisha shughuli zake, na kuipa kila inacho hitaji katika utekelezaji wa miradi yake muhimu, tunawaahidi kua tupo pamoja nao na tunawaahidi kuwasaidia Insha-Allah”.
Kumbuka kua mashirika yanayo iwakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho haya ni: Shirika la teknolojia ya kisasa na vifaa vya viwandani Aljuud, mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s), Kiwanda cha Waahah kinacho tengeneza chakula cha kuku, kiwanda cha kutotolea mayai ya kuku, ambao wanaeleza mipango ya Atabatu Abbasiyya tukufu na bidhaa wanazo tengeneza, zinazo saidia kujenga taifa kwa kiwango kinacho endana na maendeleo ya zama hizi, pia ni fursa ya kuangalia maendeleo ya kisasa yaliyopo katika taasisi zingine katika sekta ya kilimo, sambamba na kubadilishana uzowefu katika mambo ya kilimo kwa ujumla.