Maahadi ya Quráni tukufu inafanya nadwa ya Quráni katika Chuo kikuu cha Qaasim Alkhadhiraa

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha miradi ya Quráni inayo lenga makundi tofauti katika jamii, na kundi la wanafunzi wa chuo hupewa umuhimu mkubwa katika miradi yake, ukiwemo mradi wa Quráni katika vyuo vikuu na Maahadi, unaolenga kuimarisha utamaduni wa kusoma Quráni kwa wanafunzi, na kuwafanya waweze kufasiri kwa vitendo mafundisho ya Quráni tukufu katika maisha yao ya nyumbani na chuoni, huandaa semina au makongamano kuhusu Quráni na kwa kuangalia umri wa washiriki pamoja na uwezo wao kielimu.

Chuo kikuu cha Qaasim Alkhadwiraa kilichopo katika mkoa wa Baabil kimekua moja ya vituo vya mradi huu, ulio anza mwanzoni mwa muhula wa wasomo ya mwaka huu, nadwa inafanyika chini ya anuani isemayo (Quráni tukufu na athari yake katika uwanja wa kielimu na kijamii), mtoa mada alikua ni ustadhi Ali Ahmadi, amezungumzia mambo mbalimbali akitoa ushahidi wa aya za Quráni tukufu, ikiwa ni pamoja na namna ya kuweka mikakati sahihi ya kukifanyia kazi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, na namna ya kufasiri kwa vitendo mafundisho yake, na kutofanya hivyo huwa na matokeo mabaya, akasisitiza kuwa, tunatakiwa kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu daima, katika kila jambo kwenye maisha yetu, na inatakiwa zionekane athari za kushikamana kwetu na Quráni katika tabia zetu.

Kumbuka kua nadwa hii ni miongoni mwa miradi ya Quráni inayo fanywa katika vyuo vikuu na Maahadi chini ya usimamizi wa Mashekh na maustadhi walio bobea, huendeshwa kwa kiwango kinacho endana na uwezo wa elimu za wanafunzi, huchaguliwa mada maalumu ambayo hufafanuliwa kwa aya na hadithi za Mtume na Maimamu wa Ahlulbait (a.s), baada ya kutolewa mada hiyo hufunguliwa mlango wa majadiliano, ambapo mara nyingi huwa ni kwa kuzungumza moja kwa moja, mwanafunzi huuliza swali au hutoa maoni yake mbele ya mtoa mada moja kwa moja, au hutumika njia ya siri, washiriki hupewa karatasi na kalamu, kisha mwenye swali au maoni huandika na kukabidhi kwa mtoa mada, naye hujimu na kutao maelezo pale anapo takiwa kuelezea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: