Hivi karibuni katika kituo cha Al-Ameed lilbuhuthi wa dirasaat chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kimechapicha idadi maalumu ya jarida la Albaahir zinazo zungumzia elimu ya mazingira na uhandisi, kufuataia kongamano lililo simamiwa na taasisi ya mazingira ya Iraq kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kulikua na jumla ya tafiti kumi na moja kutoka kwa wasomi tofauti walio shiriki kwenye kongamano hilo kutoka vyuoni na kwenye vituo vya utafiti, tafiti hizo vimejikita katika mambo ya mazingira na namna ya kuyaboresha.
Kumbuka kua jarida hili linamalengo maalum, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mawasiliano baina ya watafiti kutoka vyuo vikuu tofauti na katika vituo vya utafiti, ili kuongeza kiwango cha elimu na kupata jopo la wataalamu wanao fanya tafiti bega kwa bega, pamoja na kubaini maeneo ya kufanyiwa utafiti, na kuweka mazingira ya kushindana baina ya watafiti, sambamba na kulifanya jarida la Albaahir kuwa na tafiti za kielimu zenye hadhi ya kimataifa, zinazo husu mambo ya kimazingira na kiuhandisi, lengo ni kushughulisha fikra na akili kwa ajili ya kunufaisha jamii ya wasomi hasa katika mambo yanayo nufaisha jamii ya watu wa sekula, kupitia jarida hilo tutaweza kusambaza tafiti za kielimu. Kuwasiliana na ofisi ya jarida hili na kuangalia idadi yake, tembelea toghuti hii: https://albahir.alkafeel.net