Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya darasa mjadala kwa wanafunzi wa bweni katika chuo kikuu cha Basra.

Maoni katika picha
Bado Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha Dini, inaendelea na program ya darasa mjadala kwa wanafunzi wa vyuo na Maahadi wanao ishi kwenye mabweni, pamoja na kutumia makongamano na mikutano ya wanafunzi inayo fanywa ndani ya majengo ya chuo, kwa kuwasiliana na uongozi wa kila chuo.

Hivi karibuni Ataba tukufu katika (kongamano la mzaliwa wa ndani ya Alkaaba), walilo liandaa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Basra, imefanya darasa mjadala kwa wanafunzi wanao ishi bwenini (kwenye nyumba za wanafunzi), lililo ongozwa na Sayyid Muhammad Mussawi kutoka kitengo cha Dini, darasa hilo lilikua na anuani isemayo: (Kiongozi wa waumini (a.s) na nguvu yake ya mvuto na ulinzi), alielezea vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - Tunajaribu kuchota japo kidogo miongoni mwa fadhila za nuru hii tukufu ya kiongozi wa waumini (a.s).
  • - Mtume (s.a.w.w) anasema: (Ewe Ali! Mimi na wewe ni mababa wa umma huu) hii inamaanisha kua baba yetu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na kiongozi wa waumini (a.s), na ibada zetu huonyeshwa kwao kila siku.
  • - Kukaa kwenu hapa mnaingiza furaha katika roho ya kiongozi wa waumini (a.s).
  • - Uislamu umefika kwetu kwa jihadi, kumwagika kwa damu, maumivu, machozi, vita nyingi, na yote hayo kiongozi wa waumini (a.s) alikua mstari wa mbele.
  • - Mmoja wa waandishi wa kinaswara kutoka Marekani ya kusini anasema: Nimeupenda uislamu na nimeingia kwenye dini hii, na nimemchagua Ali bun Abu Twalib kwa sababu kuna hoja za wazi kuwa yeye ndiye mtu wa karibu zaidi na Mtume (s.a.w.w), na ninafuata mwenendo wa Ali bun Abu Twalib (a.s).
  • - Mtu wa karibu zaidi na Mtume (s.a.w.w) kwa ushahidi wa watu wa mbali ni Ali bun Abu Twalib (a.s).
  • - Kiongozi wa waumini (a.s) alisujudu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata nafasi ya kulala kwenye kitanda cha Mtume (s.a.w.w), sajda hiyo ina maana nyingi.
  • - Mwenyezi Mungu mtukufu aliwapongeza malaika wake kutokana na msimamo wa kiongozi wa waumini (a.s) wa kulala kwenye kitanda cha Mtume (s.a.w.w).

Mwishoni mwa kikao hicho wanafunzi wakapewa karatasi ili waandike maoni yao na maswali, yanayo husu darasa mjadala (nadwa) au mambo mengine, na Sayyid Mussawi akajibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi katika yale aliyo takiwa kufafanua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: