Hivi ndio inavyo changia Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuboresha na kusambaza aina bora za kondoo.

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya miradi mingi, miongoni mwa miradi hiyo ni ile inayo husu sekta ya kilimo na ufugaji wa wanyama, na inaipa umuhimu mkubwa, imefanya kazi kubwa katika kuziendeleza sekta hizo ambazo serikali inazipuuza na kuzidharau, miongoni mwa miradi ya ufugaji ni ule wa kitua cha Abulfadhil Abbasi (a.s), cha ufugaji wa kondoo chini ya kitengo cha kilimo na ufugaji wa wanyama cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kitoa hiki kimewekwa kila aina ya vifaa vya kisasa na kimetimiza masharti yote ya ufugaji wa kitaalamu, na kua miongoni mwa vituo bora zaidi vya ufugaji wa kondoo hapa nchini.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kituo hiki mtandao wa Alkafeel umeongea na rais wa kitengo cha kilimo na ufugaji wa wanyama Mhandisi Ali Muz’ali ambaye amesema kua: “Kituo hiki kilianzishwa mwaka wa (2011m) kinalenga kuinua ufugaji wa wanyama, kwa kufuga aina bora zaidi ya kondoo, wakiwemo kondoo wa aina ya naimi, na awasi pamoja na aina zingine”.

Akaongeza kua: “Tulianza na kondoo (740) leo tunamshukuru Mwenyezi Mungu tuna kondoo nyingi sana, tumefikia lengo la kuanzishwa kwa mradi huu, tunaeleza kwa ufupi shughuli tunazo fanya kama ifuatavyo:

  • 1- Kulinda aina nadra za kondoo na kuhakikisha zinakua nyingi.
  • 2- Kufanya majaribio ya kielimu yenye mafanikio kwa ajili ya kupata aina bora zaidi, kwani hiki ni kituo cha utafiti na shamba la majaribio mbalimbali.
  • 3- Kutumia wataalamu wenye uzowefu mkubwa katika sekta hii.
  • 4- Kuingiza nyama nzuri katika soko la ndani, tunachangia kati ya asilimia (%10-15) kwenye soko la Karbala na Najafu, na tunauza kwa bei nafuu kwa ajili ya kusaidia familia za mafakiri ziweze kununua nyama hizo.
  • 5- Kufuga na kuingiza aina mpya za kondoo na kuzitunza kwa ajili ya kuzifanya ziwe nyingi kutokana na mazingira ya Iraq.
  • 6- Kuchangia katika kuendeleza kondoo wa kienyeji na kuhakikisha wanakua wengi kwa ajili ya kuboresha uchumi wa taifa.
  • 7- Kufuga kwa wingi aina zinazo pendwa na vituo vya serikali pamoja na wafugaji wengine pia.
  • 8- Kusaidia mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu uweze kupata nyama kwa bei nafuu ukilinganisha na ongezeko la wageni wanao ingia kwenye mgahawa (mudhifu) huo.
  • 9- Kuweka mikakati ya kuboresha kondoo wa kienyeji kwa kutumia utalamu wa kisasa hasa aina zinazo pendwa na watu.
  • 10- Kituo kinatoa ushauri na maelekezo ya kitaalamu kuhusu ufugaji wa kondoo”.

Akabainisha kua: “Eneo unapo fanyiwa mradi huu linaukubwa wa (dunam 450) -sawa na heka 225 takriban- katika jangwa la Karbala, limegawanywa sehemu (mazizi) kumi ya mbuzi na kondoo za aina mbalimbali, kila zizi linaukubwa wa mita za mraba (1600), pia limewekwa mambo yote muhimu na yalazima, na tumeandaa mashamba maalumu ya majani kwa ajili ya mifugo hiyo”.

Akasisitiza kua: “Kiwango cha uzaaji kwa mwaka ni zaidi ya (1600), tuna aina bora ya mbuzi tunazo chagua kuzitoa uzazi, zowezi hilo hufanywa chini ya madaktari walio bobea pamoja na mtaalamu wa chakula cha mifugo, kila mmoja hutoa maoni yake kulingana na fani yake”.

Akaendelea kusema kua: “Kitua kina godauni la chakula cha mifugo, pia kuna kiwanda cha kutengeneza vyakula vya mifugo, pia kuna mabaki ya mitende na mengineyo, kazi zote zinafanywa kwa utaalamu na umakini wa hali ya juu, ili tuweze kupata kondoo wenye uzito mkubwa na ubora wa haji ya juu, pia kuna mashine za kusukuma maji, mashine hizo ni muhimu sana hasa wakati wa kiandazi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: