Rais wa muungano wa wabunifu wa kiiraq: Tunatakiwa kuangalia kwa makini namna ya kuwasaidia wabunifu na kumaliza sintofahamu.

Maoni katika picha
Jioni ya Jumatano (12 Rajabu 1440h) sawa na (20 Machi 2019m) rais wa muungano wa wabunifu wa kiiraq Ustadh Zaiduna Khalfu Saidiy, amehutubia katika ufunguzi wa kongamano na maonyesho ya pili ya wabunifu, linalo endeshwa na wabunifu kwa ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Karbala ni kitovu cha elimu na wanachuoni) litadumu kwa muda wa siku tatu.

Katika ujumbe wake amesema kua:

“Kwanza kabisa natoa pongezi kwa kuadhimisha kuzaliwa kwa mwalimu wa uislamu Imamu Ali (a.s), kutokana na elimu yake tumeweza kutafakari na kugundua vitu, hakika ni fahari kubwa kwetu Atabatu Abbasiyya tukufu kujitolea kufadhili kongamano hili chini ya kauli mbiu isemayo (Karbala ni kitovu cha elimu na wanachuoni)”.

Akaongeza kua: “Kongamano hili linaonyesha mwamko walionao wadau wa elimu na walezi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hususan sisi watu wa dunia ya tatu ambao utafiti wa kielimu ni muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi wetu, na ndio sababu kubwa ya kuweka malengo endelevu, bali ndio nyenzo kubwa ya kubadilisha harakati nyingi za kibinaadamu, pia ni moja ya nguzo za uchumi, na nyenzo muhimu katika misingi yote mitatu, msingi wa maendeleo ya tafiti za kielimu, au katika sekta ya uzalishaji na upande wa jamii”.

Akafafanua kua: “Leo hii baada ya kila kilicho fanywa na muungano wa wabunifu wa kiiraq ndani ya miaka minne iliyo pita, kutokana na kushiriki katika mahafali ya kitaifa na kimataifa, imekuwa ni lazima kwetu kujibu maswali matatu ya msingi yafuatayo.

Kwanza: Jambo gani halina maendeleo katika mfumo wa tafiti hapa Iraq?

Pili: Mbunifu wa kiiraq ananafasi gani katika ulimwengu wa teknolojia?

Tatu: Nini wasaidiwe wabunifu na wanawezaje kuonyesha matokeo halisi ya ubunifu wao?”.

Akasema kua: “Muungano wa wataalamu wa Iraq ulikabidhi mapendekezo yake kwa waziri mkuu, kuhusu: (Mkakati wa taifa katika ubunifu), ndani ya kipindi cha miaka mine ukiwa na vipao mbele vifuatavyo:

Kwanza: “Kufanyia kazi kanuni ya ubunifu namba 31 ya mwaka 1930m na vipengele vinavyo fuata, vinavyo husu kuiingiza Iraq katika nchi za kimataifa zenye uwezo wa kufanya ubunifu, na mkataba wa Parisi wa mwaka 1976m.

Pili: Ushiriki wa kitaifa utakao waweka katika mazingira bora wabunifu na kuwa sawa na wabunifu kutoka: Ujerumani, Kanada, Romania, Polandi, Uturuki, Iran, Misri na Kuwait, chini ya vigezo vya kimataifa.

Inatulazimu kutazama kwa makini jambo hili na kulisapoti, tumalize sintofahamu, tuangalie ubunifu kwa makini na tuhakikishe unaleta mafanikio ya wazi”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunatoa shukrani nyingi kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kutukaribisha mara ya pili katika mjumuiko huu mtukufu, na tunaishukuru kamati ya majaji iliyo fanya kazi kubwa ya kuchambua na kuthaminisha aina mbalimbali za ubunifu na hatimae kuja na aina themanini zilizo pasishwa katika sekta za vifaa tiba, dawa, ujenzi na uhandisi, pamoja na sekta ya kurutubisha yeruniam, kemikali, mbolea na vifaa vya ulinzi na usalama, tunajitahidi kuona kila kinacho onyeshwa katika maonyesho haya kinaingia katika hatua ya utendaji na kulitumikia taifa letu kipenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: