Chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu: lafanyika kongamano na maonyesho ya pili ya ubunifu.

Maoni katika picha
Ndani ya ukumbi wa mikutano katika jengo la Shekh Kuleini (q.s), Alasiri ya Jumatano (12 Rajabu 1440h) sawa na (20 Machi 2019m), umefanyika ufunguzi wa kongamano na maonyesho ya pili ya wabunifu, yanayo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Karbala ni kitovu cha elimu na wanachuoni) linalo endeshwa na muungano wa wabunifu wa Iraq chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu tarehe (20-22 Machi), likihudhuriwa na wasomi wengi wa sekula.

Hafla ya ufunguzi imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) pamoja na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqari (d.t) na wajumbe kadhaa wa kamati kuu ya uongozi, hafla imefunguliwa kwa Quráni tukufu halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukasomwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu uitwao (Lahnul-Iba). Halafu ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i).

Baada yake akazungumza rais wa muungano wa wabunifu wa Iraq Ustadh Zaiduna Khalfu Saaidiy.

Halafu ukafuata ujumbe wa rais wa mamlaka ya vipimo na udhibiti wa ubora ulio wasilishwa kwaniaba yake na Ustadh Muhammad Zidani Hussein, amabye amesema kua: “Katika makongamano kama haya huwa tunazingatia sana kupata matokeo halisi na kuweka mikakati madhubuti ya kuwasaidia wabunifu”. Akaongeza kua: “Tunawashukuru wasimamizi wa kongamano hili, na sisi katika mamlaka ya taifa ya vipimo na kudhibiti ubora tupo tayali kutoa msaada wowote kwa wabunifu wetu”.

Mwisho wa hafla watu wote walio hudhuria walielekea katika ufunguzi wa maonyesho ya kazi za ubunifu zinazo shiriki katika maonyesho haya yanayo fanyika kwa mara ya pili, kazi zinazo shiriki katika maonyesho haya zinahusu vifaa tiba, dawa, vifaa vya ujenzi na zana za kihandisi, pamoja na vifaa vya viwandani, kemikali, mbolea na vitu vinavyo husiana na sekta ya ulinzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: